Mke wa zamani wa Chameleone aeleza sababu ya kutomuomboleza shemeji yake, Humphrey Mayanja

Ufafanuzi huu kutoka kwa Daniella umezua mijadala kwenye mitandao ya kijamii, huku watumiaji wengi wakimkosoa kwa kutoonyesha kuifariji familia hiyo katika wakati mgumu.

Muhtasari

• Mayanja alifariki na kuzikwa wiki jana baada ya kuugua kwa muda kutokana na gonjwa la saratani.

• Hata hivyo, baadhi ya watu wamejitokeza kumtetea Daniella, wakidokeza kwamba huenda alikuwa na sababu za kibinafsi za uamuzi wake wa kutohusika katika mazishi ya Humphrey

familia ya Jose Chameleone
familia ya Jose Chameleone
Image: Maktaba, Facebook

Daniella Atim, aliyekuwa mke wa msanii nguli kutoka Uganda, Jose Chameleone kwa mara ya kwanza amefunguka sababu zilizopelekea kimya chake chenye kishindo kikubwa baada ya kifo cha kakake mkubwa kwa Jose Chameleone, Humphrey Mayanja.

Mayanja alifariki na kuzikwa wiki jana baada ya kuugua kwa muda kutokana na gonjwa la saratani.

Baada ya kifo chake, watu mbalimbali walipeleka kwenye mitandao ya kijamii kumuomboleza Mayanja na wengine kutuma risala za rambirambi kwa familia ya Chameleone kwa kumpoteza kakake mkubwa ambaye pia aliwahi kuwa meneja wake.

Hata hivyo, Daniella Atim hakuweza kumuomboleza Mayanja kwa ujumbe wowote wala kuandika chochote kumhusu katika kipi ndi cha maombolezo, jambo ambalo liipelekea baadhi ya wanamitandao kutaka kujua kwa nini hakuonesha utu kwa marehemu.

Daniella alijibu mtu mmoja aliyemtupia swali kama hilo kwenye ukurasa wake wa Instagram, akitoa sababu kwamba hakumuomboleza kwa kile alichokitaja kuwa marehemu hana uwezo wa kuona kama ameombolezwa au la.

"Mlifiwa kama familia, lakini hata ujumbe wa kumuomboleza hukufanya?" mmoja alimuuliza.

Akijibu, Daniella Atim alisema, "Kwani wewe hujui kwamba wafu hawawezi kusoma ujumbe!"

daiella atim
daiella atim

Ufafanuzi huu kutoka kwa Daniella umezua mijadala kwenye mitandao ya kijamii, huku watumiaji wengi wakimkosoa kwa kutoonyesha kuifariji familia hiyo katika wakati mgumu.

Hata hivyo, baadhi ya watu wamejitokeza kumtetea Daniella, wakidokeza kwamba huenda alikuwa na sababu za kibinafsi za uamuzi wake wa kutohusika katika mazishi ya Humphrey.

Baadhi wamekisia kuwa huenda kulikuwa na masuala ambayo hayajatatuliwa au mvutano kati ya Daniella na Humphrey ambao ulisababisha uamuzi wake wa kukaa mbali na kipindi cha maombolezo.