Umoja wa Afrika wamteua Uhuru kuongoza waangalizi wa uchaguzi Afrika Kusini

Taifa linajiandaa kuandaa uchaguzi mkuu Mei 29

Muhtasari

• Jukumu la msingi la timu  hilo litakuwa kutoa ripoti ya uchanguzi bila upendeleo.

Rais mstaafu Uhuru Kenyatta
Rais mstaafu Uhuru Kenyatta
Image: Hisani

Tume ya Umoja wa Afrika (AUC) imetangaza kumteua Rais mstaafu Uhuru Kenyatta kuongoza timu ya waangalizi waliopewa jukumu la kusimamia uchaguzi mkuu ujao nchini Afrika Kusini. 

Uhuru ataongoza waangalizi wa Uchaguzi huo kuanzia Mei 21 hadi Juni.  Afrika kusini linajiandaa kwa uchaguzi mkuu Mei 29.

Jukumu la msingi la timu  hilo litakuwa kutoa ripoti ya uchanguzi bila upendeleoHii ni pamoja na kiwango ambacho uendeshaji wa chaguzi unakidhi viwango vya kikanda, bara na kimataifa vya uchaguzi wa kidemokrasia.

Pia itatoa mapendekezo ya uboreshaji wa chaguzi zijazo kulingana na matokeo.

"AUEOM itashirikiana na washikadau kadhaa na kuangalia maandalizi ya mwisho na mchakato wa upigaji kura. Kulingana na matokeo, itatoa taarifa yake ya awali baada ya siku ya uchaguzi.

Ikiwa ni sehemu ya majukumu yake, imepewa jukumu la kuonyesha mshikamano na uungaji mkono wa AU kuelekea uchaguzi na mchakato wa demokrasia nchini Afrika Kusini ili kuhakikisha kuwa uchaguzi wa kidemokrasia, wa kuaminika na wa amani unachangia uimarishaji wa utawala wa kidemokrasia, amani na utulivu nchini humo.

Ujumbe wa waangalizi unatoa mamlaka yake kutoka kwa vyombo mbalimbali vya AU, hususan miongozo ya AU ya ujumbe wa uchunguzi na ufuatiliaji wa uchaguzi (2002), na Azimio la OUA/AU kuhusu Kanuni Zinazosimamia Uchaguzi wa Kidemokrasia Afrika (2002).

Pia inatokana na Mkataba wa Afrika wa Haki za Binadamu na Watu (1981) na Mkataba wa Afrika wa Demokrasia, Uchaguzi na Utawala (2007).

AUEOM pia inawiana kuhakikisha utawala bora, demokrasia na kuheshimiwa kwa haki za binadamu, haki na utawala wa sheria.