Mkuu wa polisi aiba bunduki ya mdogo wake na kuichukulia mkopo rahisi wa Ksh 25k

Bunduki hiyo aina ya AK 47, ikiwa na risasi 30 ilipatikana siku 10 baadae chini ya umiliki wa mtoaji mikopo rahisiikiwa bado hajatumika.

Muhtasari

• Hata hivyo, ilipatikana siku 10 baadaye, kutoka kwa mkopeshaji fedha katika Bunabude jirani - ambaye inaonekana alikuwa ameibeba kama fimbo kuonyesha uwezo wake mpya.

Bunduki
Bunduki
Image: Andrew Kasuku

Bosi wa polisi katika kituo cha polisi cha Lusha, eneo la Elgon wilaya ya Bulambuli nchini Uganda ametuhumiwa kuchukua bunduki ya mdogo wake kisha kuiweka rehani kwa shilingi za Uganda, 700k sawa na shilingi 25k pesa za Kenya.

Kwa mujibu wa Nile Post, bosi huyo wa polisi aliichukua bunduki hiyo na kuiweka kama dhamana ya mkopo wa masharti nafuu.

Bunduki hiyo aina ya AK 47, ikiwa na risasi 30, iliyokuwa imetumwa katika Kituo cha Polisi cha Lusha katika Kitongoji cha Lusha vijijini, ilitoweka Aprili 10 katika mazingira ya kutatanisha, jarida hilo liliripoti.

Hata hivyo, ilipatikana siku 10 baadaye, kutoka kwa mkopeshaji fedha katika Bunabude jirani - ambaye inaonekana alikuwa ameibeba kama fimbo kuonyesha uwezo wake mpya.

Mazingira ambayo mkopeshaji pesa, aliyetambulika tu kama Sande, alipata bunduki nyuma ya mabega yake yalifichuka Jumatano iliyopita wakati Kamanda wa Polisi wa eneo la Elgon Bosco Otim Loro alipotangaza kuwa bunduki hiyo ilikuwa imepatikana ikiwa vile ilivyokuwa.

"Kwa kweli, bunduki haikupotea, ilitolewa na afisa wa polisi badala ya pesa," mzee katika kijiji cha Lusha aliambia gazeti la Nile Post kwa kujiamini.

Ilikuwa kwa mkopo wa Shs700,000, Nile Post ilibaini.

Uchunguzi uliofanywa baadae umebaini kuwa wakati bunduki hiyo haijaweza kufahamika ilikotokea askari aliyetia saini yake alizuiliwa.

Polisi huyo, katika maelezo yake, alifichua kuwa bunduki hiyo ilitoweka nyumbani kwake. Mkewe baadaye alichukuliwa na uchunguzi ukazidi.