"Sijawahi enda klabuni," Harry Kane azungumzia maisha yake kando na soka

"Sijawahi kuwa mtu ambaye huenda nje kwa vilabu vya usiku. Ninapokuwa na muda, napenda kuutumia na mke wangu na watoto wangu, napenda kucheza gofu."

Muhtasari

• Mshambuliaji huyo wa England mwenye umri wa miaka 30 ana msimu mzuri wa kwanza katika ligi ya Ujerumani.

Harry Kane
Harry Kane
Image: Facebook

Mshambuliaji wa Bayern Munich ambaye pia ni nahodha wa timu ya taifa ya Uingereza, Harry Kane amefichua ratiba ya maisha yake kando na soka.

Katika mahojiano yaliyochapishwa na jarida la GOAL.com, Harry Kane alisema kwamba kando na soka, maisha yake ni ya kawaida tu kama mtu yeyote.

Alifichua kwamba wakati akiwa na muda mbali na soa, hutumia muda huo kukaa na familia yake wala hajawahi hata siku moja kufikiria kwenda katika vilabu vya vileo kujistarehesha.

"Ninapenda kuweka mambo ya faragha na nadhani yote hayo yanategemea aina ya mtu niliye. Mimi ni mtu wa kawaida na ninafanya mambo ya kawaida. Sijawahi kuwa mtu ambaye huenda nje kwa vilabu vya usiku. Ninapokuwa na muda, napenda kuutumia na mke wangu na watoto wangu, napenda kucheza gofu."

Mshambuliaji huyo wa England mwenye umri wa miaka 30 ana msimu mzuri wa kwanza katika ligi ya Ujerumani, na kuvunja rekodi nyingi za Bundesliga baada ya mechi 18 pekee za Bavarians.

Bayern walitumia kitita cha Euro milioni 100 kumnunua Kane msimu huu wa joto na fowadi huyo wa Uingereza anatumai kushinda taji lake la kwanza kuu akiwa na The Bavarians baada ya kushindwa katika harakati zake za kushinda mataji akiwa na Tottenham.

Juhudi za mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 30 zimesaidia vijana wa Thomas Tuchel kilele cha kundi lao la UCL wakiwa wamebakisha michezo miwili, kwani tayari wamejikatia tiketi ya raundi ya muondoano.