Ligi ya Mabingwa: Magoli 2 ya Vinicius yaisaidia Real Madrid kutoka sare na Bayern Munich

Real wanarudi katika uwanja wa nyumbani wa Bernabeu katika mechi ya mkondo wa pili Jumatano ijayo.

Muhtasari

•Mbrazil huyo alichukua fursa ya makosa mawili ya beki wa Bayern Kim Min-jae - kumpita kwa kasi na kuachia shuti lililompita kipa Manuel Neuer.

•Udhibiti wa mchezo ulibadilika baada ya Bayern kushindwa kuchukua fursa kabla ya Vinicius kupokea pasi safi kutoka kwa kiungo Toni Kroos .

Image: BBC

Vinicius Junior alifunga mabao mawili na kuisaidia Real Madrid kutoka sare katika mechi ya kwanza ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Bayern Munich.

Mbrazil huyo alichukua fursa ya makosa mawili ya beki wa Bayern Kim Min-jae - kumpita kwa kasi na kuachia shuti lililompita kipa Manuel Neuer, kabla ya raia huyo wa Korea Kusini kumfanyia madhambi Rodrygo kwenye eneo la hatari na Vinicius kufunga penalti hiyo.

Nahodha wa Uingereza, Harry Kane alikuwa amefunga penalti ya aina yake, akimshinda mlinda lango Andriy Lunin mapema kipindi cha pili baada ya Jamal Musiala kuangushwa na Lucas Vazquez kwenye eneo la hatari.

Dakika chache kabla, mchezaji mwenza Leroy Sane alikuwa amepiga shuti kali ndani ya lango la Bayern, na kusawazisha bao la kwanza la Vinicius.

Udhibiti wa mchezo ulibadilika baada ya Bayern kushindwa kuchukua fursa kabla ya Vinicius kupokea pasi safi kutoka kwa kiungo Toni Kroos .

Wakiwa wameshambulia mara sita na kumiliki mpira kwa zaidi ya 60% katika dakika 20 za kwanza - nafasi nzuri zaidi za Bayern ziliwaangukia Sane na Kane – lakini Bayern walijikuta nyuma.

Lakini kipindi kibaya cha dakika nne katika kipindi cha pili kiligeuza mchezo na wababe hao wa Ujerumani kurejesha kasi yao.

Waliiweka Real chini ya shinikizo na labda walikuwa na bahati mbaya kutokuwa kifuo mbele .

Kosa la Kim - kuvuta shati la Rodrygo bila sababu katika dakika ya 83 - liliwaruhusu Real kurejea mchezoni na sasa wanarudi katika uwanja wa nyumbani wa Bernabeu katika mechi ya mkondo wa pili Jumatano ijayo.