(+ Video ) Wanaume wawili wasuguana na kukata viuno, wengi washangaa

Screenshot_from_2019_12_01_14_16_37__1575199851_50764
Screenshot_from_2019_12_01_14_16_37__1575199851_50764
Kipande cha video kinachoonyesha majamaa wawili wakisuguana na kukata viuno kimewashangaza wengi katika mitandao ya kijamii.

Wengi wakiajabia tukio hilo na ambalo ni mwiko kwa jamii nyingi hapa nchini.

Wawili hawa walikuwa katika fiesta ya Nai Fest iliyoandaliwa Ngong Road jana usiku.

https://www.instagram.com/p/B5hjyTIFga_/

Je, video kama hii inaashiria nini haswa?

Watu katika mitandao ya kijamii wamezungumza sana huku Hanifa_moha akisema kuwa anatamani sana angekuwa na furaha kama hawa 'wapenzi'.

hanifa_moha" I wish I was happy like these two lovers 😘😘😘😘..."

Tamko hili linazua kisa cha mahusiano ya jinsia moja.

 Jamii nyingi Afrika bado hazijakubali ndoa au hata mahusiano ya jinsia moja.

Katiba na sheria nchini zinasalia kimya katika swala la jinsia moja kuhusika katika mahusiano.

Dhana kubwa ni kuwa mashoga na wasagaji wanafanya kitu na ambacho si halali.

Madhehebu mbalimbali yamekashifu uwepo wa makundi hayo.

"Kuna visa vingi vya kushurutishwa na polisi na hata kubaguliwa, baadhi ya watu huogopa kuja hapa maana hawajui kinachoweza kuwapata. Polisi wanaweza kuvamia na kukamata watu'' Alifichua kasisi mmoja.

Kasisi mmoja amenukuliwa kusema kuwa haki yao ni muhimu zaidi,

"Kuondolewa kwa sheria hizo kutawapa ujasiri na kufahamu kuwa si washukiwa na hivyo kuwawezesha kuhusiana na watu bila woga,’’ aliongozea.