Wawili Waaga Baada Ya Bodaboda Kugongana Na Gari Barabara Ya Voi-Mwatate

Watu wawili (wanaume),mwendesha bodaboda na abiria wake wameaga dunia mapema leo baada ya kugongana ana kwa ana na gari dogo aina ya Totoya Wish eneo la Landi barabara ya Voi-Mwatate kaunti ya Taita Taveta.

Akidhibitisha ajali hiyo OCPD wa Mwatate, Francis Mwangi, amesema wawili hao waliaga papo hapo baada ya kugonga gari hilo dogo.

Mwangi amewataka madereva wanaotumia barabara hiyo kuwa waangalifu.