Visa hivyo ni kutoka sampuli 4,888 zilizopimw akatika saa 24 zilizopita .
Waziri wa afya Mutahi Kagwe amesema watu 409 ni wanaume ilhali 197 ni wanawake .mgonjwa aliye na umri wa chini sana ana miezi minne ilhai mwenye umri wa juu ana miaka 85.
Watu 75 wamepona kutokana na ugonjwa huo na kufikisha 7,908 watu waliopona corona hadi kufikia sasa .
Kagwe amesema wanaofanyia kazi nyumbani wanafaa kuhakikisha kwamba wanafanyia katika nyumba zao .
" Nimekuwa risasi nawe pia umekuwa risasi ,tumekuwa hatari na tunaweza kusababisha maafa’ amesema Kagwe
Amewahimiza wazazi kuhakikisha kwamba wanapo wananawa mikono kila wakati
Kagwe amekariri msimamo wa rais Kenyatta kwamba hakuna atakayesazwa katika kuhakikisha kwamba kila mmoja anafuata kanuni zilizowekwa kuzuia usambaaji wa virusi vya corona .
Amewashauri watu kutosafiri kwenda mashambani ama kuwaalika wageni makwao isipokuwa katika hali za dharura .