15 waaga dunia huku 497 wakipatikana na virusi vya corona

Watu 15 wameaga dunia kwa ajili ya virusi vya corona katika saa 24 zilizopita .

Katibu wa utawala wa wizara ya Afra Mercy Mwangangi  amesema hayo wakati akitangaza kwamba Kenya imesajili visa vipya 497 vya ugonjwa huo nchini  kutoka sampuli  4171 na kufikisha jumla ya visa hivyo  nchini kuwa 27425.  Kati ya waliopata ugonjwa huo 467 ni wakenya ilhali 30 ni  raia wa kigeni .

Wagonjwa  312 ni wanaume ilhali 185 ni wanawake . Mwangangi pia ametangaza kwamba 372 wamepona idadi inayofikisha jumla ya watu waliopona ugonjwa huo hadi sasa kuwa 13,867.

Kati ya watu 15 walioaga dunia ,11 walikuwa na matatizo ya awali ya kiafya na idadi hiyo sasa inafikisha 438 walioangamia kwa ajili ya virusi vya Covid 19 nchini .