Kamishona Kakamega Abdulrizak Jaldesa aelezea hofu yake idadi ndogo ya wavulana shuleni

Abdulrizak Jaldesa
Abdulrizak Jaldesa
Kamishona wa kaunti ya Kakamega Abdulrizak Jaldesa ameelezea hofu yake kutokana na idadi ndogo ya watoto wavulana kwenye shule ikilinganishwa na wasichana jambo ambalo linapelekea wengi wao kujihusisha kwa visa vya uhalifu katika eneo la Matungu.

Akihutubu kwenye hafla ya Madaraka mjini Mumias Jaldesa amewahakikishia wananchi kujitolea kwa serikali kuthibiti usalama eneo la matungu na amewataka viongozi na wazazi kushirikiana kuona kwamba watoto wavulana hawajihusishi na visa potovu.

Kwingineko

Idara ya usalama kaunti ya Taita Taveta imeimarisha hatua za kukabili ongezeko la uhalifu eneo la Taveta , mpakani mwa Kenya na Tanzania.

Kamishna wa kaunti hiyo Rhoda Onyancha anasema kwa muda sasa wahalifu wamekuwa wakitekeleza maovu mjini Taveta na kutorokea Tanzania.

 Kwingineko 

Viongozi wa Mlima Elgon kaunti ya Bungoma wakiongozwa na mbunge wa eneo hilo Fred Kapondi wamejitengana na madai ya baadhi ya wakereketwa wa kisiasa wa eneo hilo kutaka kujitenga na kaunti hio ili kujiunga katika kaunti ya Trans Nzoia.

Wakiongea hapo jana katika madhimisho ya sherehe za madara dei katika shule ya upili ya Kapsokwony viongozi hao wameelezea kuridhishwa na maendeleo yanayotekelezwa na serikali ya kaunti ya Bungoma chini ya gavana Wycliffe Wangamati na kutaja hatua ya baadhi ya wakereketwa wa kisiasa wakiongozwa na Eunice Chepchumba,Nathan Warsama pamoja na Masudi Chemaswet  wanaodai kujitenga kama porojo,uvumi na yasio na msingi wowote.

Kapondi na mbunge wa zamani John Serut wamesema kamwe hawaungi mkono mapendekezo hayo.

Haya yanajiri baada ya wakereketwa  hao kuwasilisha ombi katika bunge la senet kutaka eneo hilo kujinga na kaunti ya trans nzoia kwa msingi wa kutengwa na serikali ya Bungoma.

Soma mengine hapa