mafuta

Mkusanyiko wa Habari na Matukio Muhimu Tarehe 14 Juni 2019

  Hakimu mkuu wa  Kiambu ajiuzulu

Hakimu  mkuu wa Kiambu Brian Khaemba amejiuzulu wadhfa wake baada ya  idara ya mahakama kumsimamisha kazi kwa ukiukaji wa maadili ya utendakazi .Khaemba alijipata mashakani kwa hatua yake ya kutoa agizo la kuzuia kukamatwa kwa gavana wa Kiambu Ferdinand Waititu

  Serikali yashauriwa kutafuta njia mbadala za kutafuta pesa

Serikali inafaa kuangazia njia mbadala za kutafuta  pesa badala ya kuwategema walipa ushuru .mwana uchumi charles karisa  amesema kampuni nyingi hazikupata faida ili kuziwezesha kulipa kodi inayotosha kuafikia malengo ya serikali

 

 Aliyekuwa mkurugenzi wa Kenya Re  ahukumiwa miaka 3 jela

  Aliyekuwa  mkurugenzi  wa kifedha wa kampuni ya kenya Re  John Kinyua  amehukumiwa miaka mitatu jela  baada ya kupatikana na  hatuia ya kununua nyumba mtaani Karen  kwa njia isiofaa . mtuhumiwa mwenzake Mary Ng’ang’a   naye  amepigw afaini ya shilingi milioni sita la sivyo ahudimie kifungo cha miezi 18 gerezani . kinyua anahudumia kifungu cha miaka mitatu jela kwa kosa tofauti .

  Bei ya Petroli yapanda

Wenye magari  watagharamika zaidi mwezi huu baada ya bei ya super petrol kuongezwa kwa shilingi tatu na senti saba .katyika bei mpya zilizotangazwa na tume ya ERC  mafuta ya disel yamepanda kwa senti 39 ilhali mafuta taa yamepanda kwa  senti 34. Lita ya petrol hapa jijini itauzw akwa shilingi 115 na senti 10.

Mandagao atofautiana na waakilishi wa kaunti

Gavana wa Uasin Gishu Jackson mandago  ametofautiana na waakilishi wa kaunti baada ya kuukata mswada  ambao viongozi hao wanataka kupewa shilingi bilioni 1.5 za maendeleo . waakilishi hao wanataka kila wadi kupewa  takriban shilingi  milioni 43 .

  Mombasa kuanzisha mchezo wa gofu shuleni

Kaunti  ya Mombasa  inalenga kuanzisha mchezo wa gofu katika shule za umma za msingi .naibu  kamishna wa kaunti  Mohamed maalim  amesema mchezo huo utasaidia kuwapa nidhamu wanafunzi  .shule za kongowea ,likoni ,serani na maweni zimechaguliwa kwa mpango wa majaribio .

 

 Hakimu wa Nyeri Pauline Chesang aachiliwa kwa dhamana

 

Hakimu wa nyeri Pauline chesang  na watu wengine wanne walioshtakiwa kwa kumwua mume wake  Robert chesang wameachiliwa kwa dhamana ya shilingi laki tano .  Jaji George Odunga amewaagiza  watuhumiwa kuziwasilisha paspoti zao kortini .  Sio rahisi kugundua daalili za Ebola

  Sio rahisi kugundua daalili za ugonjwa wa ebola  kwani  hujitokeza kama magonjwa mengine .hata hivo  Daktari kutoka WHO  Richard Banda  anasema unafaa kuwa mwangalifu kuhusu daalili kama kuharisha ,kutapika na joto mwilini endapo umezuru eneo ambako kuna mchipuko wa ugonjwa huo.

 Washukiwa watatu wakamatwa Eldoret  wakiwa na  mifuko ya plastiki

 Polisi huko eldoret wamewakamata washukiwa watatu  na kunasa lori lililokuwa na mifuko ya plastiki iliyopigwa marufuku . mkuu wa DCI wa eldoret magharibi Linah Kabaillah  amesema pia wamepata shehena nyingine ya karatasi hizo katika nyimba ya mfanyibiashara mjini eldoret .

Photo Credits: The Star

Read More:

Comments

comments