Je, unafahamu athari za uonevu wa ukatili unaofanyika shuleni?

_108371882_0ae7c787-9ceb-428f-b383-876846925269
_108371882_0ae7c787-9ceb-428f-b383-876846925269

Wakati wazazi wanapowapeleka watoto wao katika shule za sekondari za malazi ,wengi wao kama si wote, huwa wanategemea kuwa maisha yao yatakuwa mema, salama na watatunzwa vema, lakini haiwi hivyo kwa baadhi.

Waliosoma shule nyingi hususan Wakati wazazi wanapowapeleka watoto wao katika shule za sekondari za malazi ,wengi wao kama si wote, huwa wanategemea kuwa maisha yao yatakuwa mema za umma katika nchi za Kiafrika zikiwemo za Afrika mashariki hali huwa ni tofauti kutokana na uonevu ambao baadhi ya wanafunzi huwa wanakabiliana nao kutoka kwa wanafunzi wenzao, na hata waalimu wao.

Uonevu huu hufanyika kwa njia tofauti, ikiwemo kudhalilishwa, kutukanwa, kuibiwa au kufichwa kwa mali zao, wakati mwingine hata kupigwa na kujeruhiwa.

Matukio ya aina hii yamekuwa yakiendelea, huku baadhi yakijulikana na mengine kutojulikana kutokana na wanaoonewa kunyamaza kwa hofu ya kushambuliwa zaidi au hata kufukuzwa shule.

Wiki iliyopita karibuni Wanafunzi 10 Umbwe Sekondari nchini Tanzania walisimamishwa masomo, kutokana na vurugu zilizotokea katika shule hiyo, na hii ilisababisha wanafunzi.

Tukio hilo lilikemewa na Waziri wa nchi ofisi ya rais tawala za mikoa Seleman Jafo akililitaja tukio hilo kama ubaguzi na mateso kwa wanafunzi, na kubainisha kuwa Serikali haitavumilia walimu wakuu wanaotajwa kuwa na tabia hizo, na akaagiza uchunguzi ufanyika juu ya wahusika.

Miongoni mwa watu waliopitia uonevu wa aina hii katika shule za sekondani ni Bwana Nickson R. Mlang'a alipokuwa akisomea shule ya sekondari ya Nyamongo . Licha ya kwamba vurugu hizi zilikuwa ni kati ya makundi mawili-kutokana na malumbano ya vidato vya chini na vidato vya juu, binafsi aliathirika kwa kiasi kikubwa:

''Vurugu zilikuwa ni kati vidato vya juu yaani cha tano na cha sita ambao walikuwa wanataka wanafunzi wa vidato vya kwanza, cha pili hadi cha nne, ni lazima tuwaheshimu na kuwafanyia kazi zao ...Kidato cha nne kikaingilia kati na kusema hilo halitawezekana ndio kukatokea malumbano na vurugu''. Alikumbuka Mlang'a katika mahojiano na BBC.

Anasema: ''Zilikuwa ni wiki mbili kabla tuanze mitihani ya Moko iliniuma sana...kutokana na vurugu tukaambiwa tutoke shuleni mara moja ...Tukaambiwa tumepangiwa kwenda shule nyingine, yaani ilikuwa ni kututawanya...sijui shule gani! , Nilikuwa Nyamongo nikahamishiwa kiboriloni, kwa hiyo hatukuwa na muda wa maandalizi ya mtihani wa Moko. Kuhamia shule nyingine kuizowea na kuzowea masomo iliniathiri sana...hili lilinitoa kabisa katika mawazo ya masomo'', anasema Mlang'a na kuongeza kuwa vurugu hizo zilichangia kuathiri ufaulu wa masomo yake.

Matukio haya ya uonevu na mateso dhidi ya wanafunzi wanaosoJe unafahamu athari za uonevu wa ukatili unaofanyika shuleni?

ma katiks shule za mara nyingine huwa ya kutisha.

Mfano nchini Kenya kisa cha mwanafunzi mwenye umri wa miaka 15- aliyekuwa akisoma kidato cha pili katika shule ya sekondari ya Nairobi School aliyedaiwa kushambuliwa kikatili kiasi cha kuuharibu ubongo wake, jambo lililoibua hisia kali miongoni mwa Wakenya.

Taarifa hiyo iliyotangazwa kwa mara ya kwanza na televisheni ya kibinafsi nchini Kenya, iliashiria ukubwa tatizo hili katika shule za umma nchini humo.

  • Mtu aliyeonewa hushindwa kujitetea na kujieleza pale anapotakiwa kufanya hivyo.
  • Uonevu huathiri watoto wa shule na hivyo kushindwa kuwa makini wawapo darasani na baadae katika maisha yao.
  • Huwa ni mtu mwenye uoga na kila mara huhisi anaonewa hata anapokuwa mtu mzima.
  • Hushindwa kuona mambo kwa mtizamo hasi na kushindwa kuchukua maamuzi ya kujitetea
  • Na hata anapokuwa katika mahusiano ya ndoa mtu aliyeonewa huenda amuonee mwenza wake

Mwanasaikolojia Perpetual Wanyugi anashauri iwapo mtoto wa shule atabainika kuwa na uonevu wa ukatili unaorudia rudia anahitaji kufundishwa nidhamu, apewe msaada wa nidhamu ya wazazi na hata majirani na pale inapozidi atafutiwe msaada wa kisaikoloji.