Taarifa ya Habari Toleo la Saa Moja Jumatatu7/10/2019

RADIO JAMBO MIC
RADIO JAMBO MIC
Polisi  huko Eldoret wamewakamata washukiwa saba  wanaohusika na wizi wa magari huko Rift valley .Kamanda wa polisi wa Uasin Gishu  Johnston Ipara  amesema washukiwa hao walikamatwa  katika maeneo ya Eldoret ,Kericho , na bomet  na jumla ya magari manen  kunaswa kutoka makaazi yao.

Joseph Kori amekosa kutoa ushahidi  dhidi ya mpenzi wake wa pembeni Judy Wangui kuhusu mauaji ya mkewe  kwa sababu ya hitilafu ya ushahidi . Kori atafika kizimbani juni mwaka ujao kutoa ushahidi dhidi ya Wangui .awali alikuwa amekamatwa kuhusiana na mauaji hayo lakini sasa ni shahidi wa serikali .

Eneo la kivuko cha feri  limetangazwa kuwa eneo maalum la oparesheni ya kijeshi  na wananchi hawaruhusisi kufika hapo huku shughuli ya kuitafuta miili ya  Mariam kighendi na mtoto wake ikiendelea . mwenyekiti  wa bodi ya huduma za feri Dan mwazo  amesema eneo hilo sasa lipo chini ya jeshi la majini na  shirika la  feri .

mbunge wa Mvita  Abdulswamad Nassir  amesema maandamano dhidi ya  reli ya SGR yataenfdelea licha ya wanadamanaji kutupiwa vitoa machozi hivi leo . amesema serikali iliwadanganya kwamba imefutilia mbali agizo kwamba mizigo yote kutoka bandari  isafirishwe kutumia  SGR ilhali huko mashinani wangali wanalazimishwa kutumia usafiri wa reli .

Mbunge wa Kapseret Oscar Sudi  amewashtumu mbunge  mteule maina kamanda  katibu wa utawala  Rachel Shebesh  na spika wa bunge la Nairobi  Beatrice Elachi  kwa kukiyumbisha chama cha jubilee .Sudi amesema  rais uhuru Kenyatta anafaa kuwachukulia hatua watatu hao ambao  wamekuwa  wakitoa matamshi ya uchochezi .