Mkusanyiko wa Habari na Matukio Jumanne 29/10.2019

 Ghasia zimezuka tena katika bunge la kaunti ya Nairobi  baada ya waakilishi wa kaunti kutofautiana kuhusu hoja mpya ya kutaka kumfurusha spika Beatrice Elachi . vurugu zilianza  wakati  waakilishi wanaomwunga mkono  Elachi walipowavamia wenzao  wanaomwunga mkono kiongozi wa walio wengi Abdi Guyo .

  Watahiniwa wote waliosajiliwa kufanya mtihani wa KCPE wataufanya mtihani huo .waziri wa elimu George magoha  amesema hakuna mtahiniwa  atakayezuiwa kuufanya mtihani huo  kwa sababu ya kudaiwa karo .

  Waziri wa usalama wa ndani  Fred matiangi amewaonya   walimu  dhidi ya kucheza kamari na maisha ya wanafunzi .hii ni baada ya   kuliona dari la darasa moja  lilikikaribia kuanguka katika shule ya msingi ya GILGIL nys  ambako alikuwa anasimamia oezi la kuanza kwa mtihani wa KCPE .

MvUA itaendelea kunyesha katika maeneo mbali mbali ya taifa katika siku tano zijazo . Stella Aura kutoka idara ya utabiri wa hali ya anga  amesema kiwango cha mvua kitazidi kuanzia siku ya jumanne . maeneo yakatoyopokea kiasi cha  cha zaidi ya milimita 30 ya mvua ni pamoja na  Siaya, Kisumu, Homa Bay, Migori, Kisii, Nyamira, Trans Nzoia ana Baringo .

Mahakama imefutilia mbali  kutekelezwa kwa  arifa  iliyotolewa na wizara ya fedha  kupunguza bajeti ya idara ya mahakama . CHAMA CHA LSK ndicho kilichowasilishwa kesi hiyo kortini  na kimeagizwa kuzikabidhi pande husika  uamuzi huo huku kesi yenyewe ikitarajiwa kutajwa  Novemba tarehe 6 kwa maelekezo zaidi .

Mtihani wa KCPE Umeanza VYEMA KATIKA MAENEO MENGI YA TAIFA  .KONTENA ZA mtihani huo hapa jijini na mombasa ziluifunguliwa kwa wakati .huko Mombasa ,waziri wa elimu George Magoha alikuwa katika shule ya msingi ya mwangala mtaani likoni kushuhudia zoezi la kufunguliwa kwa mtihani

Hata hivyo mtihani huo ulichelweshwa katika baadhi za sehemu zikiwemo kwale ,baringo  turkana magharibi na west pokot kwa ajili ya mvua kubwa .

Huku hayo yakiarifiwa ,watahiniwa wanne wa KCPE katika shule za msingi za Kyunguni  na kasikeu huko Mukaa  hawatafanya mtihani wa mwaka huu wa KCPE  BAADA YA MAjina yao kukosekana katika sjaili ya watahiniwa .huyu hapa kamishna wa kaunti Maalim Mohamed .

Mfanyibiashara  Peter Karanja  ameachiliwa kwa bondi ya  shilingi milioni nne au dhamana mbadala ya  shilingi  milioni 2 pesa taslimu . Karanja ameshtakiwa kwa mauaji ya bwenyenye Tob Cohen  .jaji Daniel Ogembo amemwagiza  karanja kutokaribia boma la Cohen na pia kusalimisha paspoti yake kortini .

Kampuni ya Kenya Power  imemteua  Bernard Ngugi  kama maneja mkurugenzi  ili kuichukua nafasi hiyo mara moja .kabla ya uteuzi wake  ,Ngugi amekuwa akihudumu kama maneja  mkuu wa uagizaji .Anaichukua nafasi hiyo kutoka kwa  Jared Othieno ambaye amekuwa akihudumu kama kaimu maneja mkurugenzi .

Maafisa wawili wakuu katika idara ya usajili wa watu wamesimamishwa kazi kuhusiana na tuhuma za ufisadi .waziri wa usalama wa ndani Fred matiangi amesema wawili hao wametajwa katika visa vingi vya ulaji rushwa ambavyo   vimelipaka doa idara hiyo .

Mwakilishi wa wanawake kaunti ya Taita Taveta Lydia Haika amewataka wakazi wa kaunti  hiyo kumkea na kutomsikiza gavana Granton Samboja na wawakilishi wadi kwenye mikutano watakayoandaa hadi pale watakapo suluhisha mzozo wa bajeti unaoendelea.Haika anasema kuwa tofauti kati ya  pande hizo mbili zimelemaza maendeleo hali anayosema kuwa imeumiza pakubwa wakaazi