Mawakili mjini Mombasa watoa wito wa utulivu baada ya kifo cha mwenzao

police
police
Shirika ya wanasheria katika kaunti ya Mombasa wameitaka umma kuwa na utulivu na kuacha kubashiri kisa na sababu cha kifo ya Sammy Anyanzwa.

Anyanzwa aliaga dunia siku ya jumatano baada ya kuanguka kutoka kwa jengo la serikali chini ya hali zisizo wazi.

Hapo awali ilidaiwa kwamba wakili huyo alijiua baada ya kujitupa kutoka kwa sakafu ya kumi ya jengo la serikali.

 Mwenyekiti wa shirika hilo la wanasheria alisema kuwa tukio hilo bado linaendelea kuchunguzwa na polisi, na pia wao bado wanangoja matokeo.

Mwenyekiti huyo aliwataka watu waachane na uvumi kwani bado ukweli ujabainika.

Vile vile alisema kuwa ni bahati mbaya watu wengine wameeneza picha za mwenzao aliyeanguka katika mitandao ya kijamii.

Mwili wa Anyanzwa ulipelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti ya Pandya.