Seneta Murkomen apewa kisomo na jaji Ogoti kuhusu tasnia ya uwakili

Sonko Lawyers
Sonko Lawyers
Kulikuwa na hali ya ucheshi na uchangamfu kwenye mahakama ya Milimani wakati seneta wa Elgeyo Marakwet Kipchumba Murkomen alipopewa kisomo na hakimu Douglas Ogoti katika uamuzi wa kesi ya gavana wa Nairobi Mike Sonko.

Murkomen alijaribu kutetea hatua yao ya kumwasilisha Sonko mahakamani, kwa kile anasema mgonjwa kuwasilishwa kortini.

"Yuko hapa kwa sababu ya amri yetu, ijapokuwa ushauri wa daktari ulisema asije....hata ingawa umetoa amri ya kumzuia ofisini lakini afya na wajibu wake kama gavana ni muhimu," Murkomen alisema.

Lakini jaji Ogoti alimuuliza sababu za kumlazimisha mgonjwa kuja kortini.

"Mbona mkamlazimisha aje kortini ilhali yu mgonjwa ?" Ogoti aliuliza.

Naye Murkomen akamjibu," Hatukutaka kubahatisha. Kuna madai mengi dhidi yake....na masimulizi kuwa ni hatari sana..."

Ogoti akamwuliza,"Ulihofia kuwa angetoroka? Najua hauna mazoea kwenye korti zetu. Haukufaa kumlazimisha mgonjwa kuja kortini kutoka hospitali. Ata bila kuwepo ningepeana tu uamuzi na hivyo malalimishi yako hayana msingi wowote." alisema.

Mazungumzo baina ya Murkomen na jaji Ogoti yaliaacha mahakama kwenye bahari ya kicheko.

Katika uamuzi wake, jaji Ogoti alimzuia Gavana Sonko kutelekeza wajibu wake kwenye afisi za kaunti huku akiachiliwa kwa dhamana ya shilingi milioni 15 au bondi ya milioni 30 Jumatano.