PATANISHO: Mke wangu aliniacha baada ya kumdanganya mke wa kwanza aliaga

Katika kipindi cha patanisho mwanaume mmoja aliyefahamika kama baba Brillian,37, alituma ujumbe ili apatanishwe na mke wake mama shalyne,29 aliyemuacha Desemba mwaka wa ,2018,

"Mke wangu alitoka nyumbani Desemba ,2018 baada ya mke wangu  wa kwanza kunipigia simu ili aongee na mtoto wake kwa maana aliniachia mtoto wake

Amekuwa akiniambia uwa tunaongea kama sipo karibu naye." Alieleza Baba Brillian.

Alizidi na kueleza sababu kamili iliomfanya mkewe aende.

" Tulipo kosana Desemba nilienda kulewa kidogo niliporudi nyumbani niliamua kimdanganya mke wangu kuwa mama Brillian ameaga dunia

Baada ya kumdanganya alikusanya virago vyake na kuenda kwa dada yake na akaniambia nifanye chochote nataka kufanya." Alizungumza.

Alisema kuwa waliachana na mke wake wa kwanza kwa sababu alikuwa na kiburi na kichwa ngumu sana.

Mama Shalyne alipigiwa simu bali hakupatikana. Je baba Brillian anapaswa kufanya nini toa maoni yako ili kumsaidia.