Visa 2 vipya vya Corona vyaripotiwa, shule kufungwa - Uhuru Kenyatta

IMG-20200315-WA0067
IMG-20200315-WA0067
Rais Uhuru Kenyatta ameagiza kufungwa kwa shule zote zisizo za bweni kufungwa kuanzia jumatatu.

Hata hivyo, shule zote za bweni zitaanza kufungwa kuanzia jumatano kufuatia mkurupuko wa ugonjwa wa Corona.

Vyuo vikuu na taasisi zina hadi Ijumaa ili kuhakikisha zimefungwa.

Rais Uhuru Kenyatta amethibitisha kuwa kuna visa viwili vipya vya virusi vya Corona.

Mwanadada ambaye alipatikana na virusi hivyo alitangamana na mgonjwa ambaye Sasa hivi ametengwa katika hospital kuu ya Kenyatta.

Serikali imepiga marufuku safari za kila mtu anayewasili nchini kutoka nchi ambazo visa vya Corona vimeripotiwa.

Ni wakenya pekee na wageni walio na stakabadhi kamili wataruhusiwa kuingia nchini lakini itawabidi wajitenge kutoka watu wengine.