Mbunge huyo alijipata mashakani kwa kumpiga risasi na kumjeruhi DJ Evolve Miezi michache iliyopita katika eneo la burudani la B Club na hadi wakati huu DJ huyo yungali amepoozwa kuanzia shingoni kurudi chini . Kumekuwa na wasi wasi kuhusu bili yake ya hospitali ambayo imeendelea kuongezeka na awali Babu alikuwa ameahidi kugharamia matibbau ya DJ Evolve .
Licha ya kuwa kwa sasa tunakabilianana janga la virusi vya Corona ,kuna wakenya ambao hawajasahau alichofanya Babu na kuja jamaa aliyejawa ujasiri na kuamua kumuuliza mbunge huyo swali hili – Mwanamme uliyejaribu kumuua yupo katika hali gani ?
Wengi walimtaraji Babu kutoka kwa makucha na kumpa pilipili jamaa huyo lakini mheshimiwa kwa upole alijibu @ndungokimanthi He’s healed in Jesus name,”
Majibizano hayo yalijiri muda mfupi baada ya Babu kutuma taarifa akisema anaunga mkono mikakati ya serikali kupambana na usambaaji wa virusi vya Corona .