21 Days! Kaunti ya Murang'a yajenga eneo la wagonjwa wa virusi vya corona kwa siku 21

EXO8oh5WsAIhY1H
EXO8oh5WsAIhY1H
NA NICKSON TOSI

Katika baadhi ya kaunti nchini, wakenya wanaendelea kuvuna matunda ya ugatuzi miaka 7 baada ya kuanzishwa. Hii ni baada ya kaunti ya Murang'a kujenge kituo cha kuwahudumia wagonjwa wa virusi vya corona kwa siku 21 na kuweka vitanda takriban 35.

Kaunti hiyo aidha imeweka mashine ya wagonjwa mahututi yaani ICU kama njia ya kujiandaa tu iwapo hali ya maambukizi ya virusi hivyo hatari vitabisha hodi katika kaunti hiyo.

Ujenzi huo sasa unawapa wakaazi wa eneo hilo matumaini ya kupata tiba bora pasi ya kuabiri hadi jijini Nairobi wakitafuta matibabu.

Ni hatua ambayo serikali kuu imekuwa ikiwataka magavana wote nchini kuhahakikisha kuwa wametenga maeneo maalum ya kuwahudumia waathiriwa wa virusi vya Corona .