3rd Force? Mudavadi akutana na Mandago Nairobi

mudavadi 1
mudavadi 1
Kiongozi wa ANC  Musalia Mudavadi jumamosi alikutana na gavana wa   Uasin Gishu Jackson Mandago  hatua ambayo imezua  uvumi kuhusu uwezekano wa kuwepo muungano wa kisiasa kati yao .

Haijabanika viongozi hao walizungumzia nini katika mkutano huo .

Wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2017 viongozi wa upinzani  wakiwemo Mudavadi  na raila odinga wa ODM waliidhinisha kuchaguliwa  KWA  Mandago kwa muhula wa pili katika mkutano wa hadhara ulioandaliwa uwanjani  64 Stadium  mjini Eldoret.

Mandago alimshinda mfanyibiashara  bilionea  Bundotich Buzeki  katika kipute kikali kuwania kiti hicho .Lakini gavana  huyo katika siku za hivi maajuzi amejitokeza kama mshirika wa karibu wa naibu wa rais William Ruto .

Duru zaarifu kwamba wawili hao walizungumza kuhusu siasa za kitaifa  ,vita dhidi ya covid 19 ,masuala ya  uchumi wan chi na ugatuzi .

Mandago amekuwa akiwahimiza wakenya kutoyachukulia kwa uzito na moyono masuala ya kisiasa .

Amesema kwamba  imekuwa mshtuko kwa waliompiga vita kiongozi wa ODM Raila Odinga ambaye sasa amekuwa mgeni wa mara kwa mara katika Ikulu .

Gavana huyo alikutana na  Ruto hivi karibuni na alikuwa miongoni  mwa walioandamana naye ili kuifariji familia ya mbunge wa zamani aliyefariki Peter Kiilu .

Mkutano wake na Mudavadi umezua mjadala wa uwezekano wa kuwepo ushirikiano wa kisiasa kati ya kambi ya Ruto na ile Mudavadi kabla ya uchaguzi mkuu wa 2022  baada ya uhusiano kati ya Ruto na rais Uhuru Kenyatta kuzorota .

Mudavadi amekuwa akikutana na viongozi kutoka maeneo mbali mbali ya nchi katika ngome yake ya   Musalia Mudavadi Centre , Nairobi anapoendelea kupiga mikakati ya kuwania urais mwaka wa 2022.