5 Wafariki huku visa vipya 141 vya covid 19 vikiripotiwa

mercy
mercy
Visa 141 vipya vya ugonjwa wa corona vimeripotiwa nchini siku ya alhamisi na kufikisha jumla ya visa vya ugonjwa huo kuwa  37,489,  katibu wa utawaka wa afya Mercy Mwangangi amesema.

Visa hivyo ni kutoka sampuli  3,307  zilizopimwa katika saa 24 zilizopita . visa vyote ni vya wakenya isipokuwa 7 .

Idadi ya walioaga dunia kwa ajili ya Covid 19 sasa imefikia watu 669 baada ya watu watano kuaga dunia .

Mwangangi amesema mgonjwa wa umri wa chini ni mtoto wa miaka mine ilhali wa umri wa  juu ana miaka 74 .

Kaunti ya Trans Nzoia kwa mara ya kwanza inaongoza kwa visa vingi baada ya kusajili visa 28 katika saa 24 zilizopita .

Nakuru ina visa  24, Nairobi 14, Migori 8, Turkana 5, Bungoma 2, Murang'a, Busia, Nyeri na Vihiga  zina kisa 1  kila moja

Watu wengine 81 wamepona na kufikisha idadi ya waliopona ugonjwa huo kuwa 24,334.

Kiwango cha uponaji wa ugonjwa huo nchini sasa kimfikia asilimia 65  . Mwangangi amesema ingawaje kenya imefaulu kupunguza maambukizi ya virusi hivyo,ugonjwa huo bado hauna tiba