Bangi hiyo ilinaswa katika boma la Martin Mungai katika eneo la Mwireri Area, Juja Farm.
Mungai alimatwa pamoja na Henry Shakira, Musa Abdi, Abdi Matayo na Brian Mwanzia siku ya ijumaa usiku
Kunaswa kwa bangi hiyo kulijiri baada ya kupatikana kwa shamba la mmea huyo katika boma hilo .
Mkurugenzi wa DCI George Kinoti amesema watano hao walijaribu kumhonga afisa mmoja mkuu wa polisi shilingi 689,000 ili waachiliwe huru .
Pesa hizo na dawa hizo za kulevya vimehifadhiwa kama ushahidi kabla ya washukiwa kufikishwa kortini .
Wiki jana seneta wa Narok Ledama Ole Kina alishauri kurekebishwa kwa sheria ili kuhalalisha utumizi wa bangi nchini kwa sababu za kimatibabu .
Seneta huyo aliisambaza viedo yake mtandaoni akiwa katika shamba la bangi nchini Lithuania .