7 wafariki huku 164 wakipatikana na Covid 19

Watu 164 wamepatina na virui vya corona baada ya sampuli 3872 kupimw akatika saa 24 zilizopita na kufikisha jumla ya visa hicho nchini kuwa 37,871 huku jumla ya sampuli zikifika 536,601.

Kutoka visa hivyo vipya 140 ni vya wakenya ilhali 24 ni vya raia wa kigeni .115 ni wanaume ilhali 49 ni wanawake .Mgonjwa wa umri wa chini ni mtoto wa miezi sita ilhali wa juu ana umri wa miaka81 .

Nairobi ndio ina visa vingi ikiwa na 41 ikifuatwa na Busia 22,Kisumu 17,Turkanba 14 ,Embu 12,Mombasa 11,Nakuru 10,West Pokot 6, Trans nzoia 5,Narok 4,Machakos 4,Uasin Gishu 4,Kilifi 3,Bungoma,2 Kiambu 2, Marsabot 2 ilhali  Kakamega ,kericho,Nandi,siaya na Taita Taveta zina kisa kimoja kila moja .

Leo watu 77 wamepona  na kufikisha idadi ya wlaiopona ugonjwa huo kuwa 24,581

Watu wengine 7 wameaga dunia kwa ajili ya ugonjwa houo na kufikisha jumla ya walioangamizwa na corona kuwa 689.