7 wafariki katika ajali ya Matulo baada ya wengine 7 kuangamia huko Malindi

Idadi ya watu waliofariki katika ajali za barabarani kuanzia jana jioni sasa imefikia watu 14 baada ya ajali nyingine kutokea mapema leo huko matulo  kwenye barabara ya  Eldoret kwenda Malaba .Ajali hiyo ilitokea wakati matatu iliyokuwa imewabeba abiria kugonga trela  ambalo lilikuwa limeegeshwa kando ya barabara .

Kamanda wa traffic Bungoma mashariki Rodgers Lwembe  amesema sita waliojeruhiwa  wanapokea matibabu katika  hospital ya kaunti ya webuye.

Jana  usiku  ajali nyingine kwenye barabara ya malindi kwenda Mombasa ilisababisha vifo vya watu saba . Ajali hiyo ilitokea wakati gurudumu  la trela moja  lilipopasuka na kulifanya kugonga matatu ya abiria .