Crime

Ajuza mwenye umri wa miaka 80 abakwa na kuauwa Kirinyaga

Polisi katika kaunti ya Kirinyaga wanachunguza kisa ambapo mwanamke mwenye umri wa miaka 80 anadaiwa kubakwa na kisha kunyongwa katika kijiji na Kianyaga.

Mwili  wa Jedida Wanjiru Wanjohi uligunduliwa na mjukumu wake mwenye umri wa miaka mitatu aliyejulisha jamaa wengine wa familia yake akisema “nyanyangu amekataa kuamka”.

Kitinda mimba wa marehemu, Stephen Weru, kisha alienda chumbani mwa mamake na kumpata akiwa mauti, uchi huku nguo zake za ndani zikiwa zimesokotwa mdomoni.

Akithibitisha kisa hicho, naibu kamishna wa Ndia Moses Ivuto alisema kwamba uchunguzi umeanzishwa, na kutoa wito kwa wananchi kutoa taarifa ili kusaidia polisi katika uchunguzi.

Wakaazi walisema kwamba hiki kilikuwa kisa cha kwanza katika kijiji hicho, na kutoa  wito kwa polisi kuhakikisha kwamba aliyehusika anatiwa mbaroni.

Mwili wa marehemu ulipelekwa katika hifadhi ya maiti ya Karatina.

TAARIFA IMEFSIRIWA NA DAVIS OJIAMBO

Read here for more

Photo Credits: File

Read More:

Comments

comments