Aamua kuokoka! Bahati amuandikia Mungu barua baada ya kushutumiwa kwa muda

NA NICKSON TOSI

Bahati jina lake linapotamkwa wengi hukumbuka baadhi ya nyimbo ambazo amezifanya na kukashifiwa na watu wanaoenzi miziki ya Injili.

Msanii huyo katika wimbo wake mpya wa Nakupa Moya aliomshirikisha msanii Akothee,ametumia fursa hiyo kumuandikia Mungu barua ya kumuomba msamaha na pia kuchukuwa fursa hiyo kumshukuru kwa mafanikio ambaye ameafikia tangu kutoka kwa makao ya kulinda watoto waliofiwa kwa jamii ya ABC Mathare.

#DEAR_GOD 😭

Nikiwa na miaka 19 nilikuwa nimeanza kutafuta kipato cha kila siku,kutoka kwa makao ya kulinda watoto waliofiwa ya ABC Mathare nikiwa sina matumaini lakini nikawa nafahamu neno lako.Umenibariki na vitu nyingi na kunitoa kwa umaskini.mwaka 2013 ulinibariki na wimbo wangu wa kwanza Mama ambao ulinifungulia milango na kubadili maisha.alisema Bahati.

Bahati anakiri kuwa amefanya makosa mengi na kutokana na hayo makosa amejifunza mengi.Vile vile ameongeza kuwa anafahamu anapigana na watu wengi ambao hawafurahii anavyoendelea kufanikiwa maishani.

“Kama binadamu ,nimefanya vitu vingi na pia nimefanya makosa mengi ambayo nimeichukulia kama funzo kwangu.mafanikio yangu yameniwezesha kuketi na wafalme na wakati mmoja kuniletea balaa na baadhi ya watu ila nakushukuru wewe Mungu kwa kunipitisha katika changamoyo hizo.aliongeza Bahati

Alihitimisha maombi yake kwa kusema kuwa hatawahi msahau Mungu tena.