Abomination! Mwanamke avua nguo na kusalia uchi mbele ya mwanawe akisherehekea birthday yake,ni sawa?

Mwanamke mmoja huko Ghana amezua gumzo mitandaoni baada ya kuamua kusherehekea birthday ya mtoto wake mvulana kwa kupiga picha naye ,akiwa uchi wa mnyama bila nguo .

Hatua hiyo ya  mwanamke huyo aliyejitambulisha katika instagram kama  Akuapem Poloo imeawaanya wanaotumia mitandao kutoa maoni mbali mbali kuhusu hatua hiyo huku wengi wakimshtumu wakisema sio sawa kufanya hivyo .

Poloo katika ujumbe wake wanasema alimzaa mtoto wake akiwa uchi na hivyo basi hamna tatizo mtoto huyo akimuona akiwa uchi pia lakini watu wengi walionekana kutofautiana naye .