Depressed

Naked and angry! Mother in-law alikuja uchi kwangu kunizomea

Sio ajabu kusikia wanawake walioolewa wakilalamika kuhusu kuwepo uhusiano mbaya na bofu kati yao na mama wakwe zao .

Lakini kwa Lucy , mama mkwe wake ,  mama ya mume  wake na nyanya ya watoto wake- alikuwa shetani!  Bifu  kati yao ilianza  pindi tu alipoolewa na  mwanzoni Lucy alikuwa mpole akidhani labda mambo yangetulia watakapozoeana na kuweza kuishi vizuri lakini wapi! Kila siku ilikuja na mapya mazito na mama mkwe hakuogopa kumuambia mwanawe kwamba hakumtaka mkewe na kwamba lazima siku moja   Lucy atafukuzwa ili mke mwingine aletwe . Tofauti zao zilikuwa kuhusu vitu vidogo vidogo ambavyo kwa watu wa nje vilionekana kama vitu vya kitoto .Kwa mfano wakati wote  mama mkwe alikuwa akiingilia masuala ya ndani ya nyumba ya Lucy .Alitaka kujua  asubuhi wamekunywa chai kwa nini ,mchana wamekula nini na jioni watapika nini ? Alitaka kujua  mbona  wamekaanga chakula  na mafuta  Fulani na sio mengine ,Mbona nguo zao zimefuliwa kwa sabuni ya  Ya kunukia .

Majuto: ‘Nilitoa mimba ya miezi sita kwa sababu mpenzi wangu alikuwa hanipi pesa’

Mama mkwe alitaka kujua  mbona wajukuu zake walikuwa katika shule Fulani na sio shule hii .kwa Ufupi Lucy alikuwa amechoshwa na  muingilio wa maisha yake  kutoka kwa mama mkwe na shemeji zake pia amboa walikuwa hawajaolewa . Siku ya siku ambapo kilele cha ugomvi wao kilifika  ,ilikuwa  siku kuu ya krisimasi ambapo  Lucy alikuwa amewaalika baadhi ya rafiki zake wa kazini kuja kwake ili washerehekee pamoja . Alitayarisha chakula kwa ajili ya wageni wake  kumbe kila  mvuto wa pilau ,chapati na mapochopocho  mengine aliokuwa akiandaa kwake  ulikuwa ukimkwaza mama mkwe ambaye alikuwa tu amengoja wageni wakiondoka aende kwa Lucy kumpa kisomo kwa kuharibu mali ya mwanawe .

Shock!Siku niliyotakiwa ‘kulala’na maiti ya mume wangu kabla hajazikwa

Wageni wapoondoka ,giza likiingia mama mkwe peupe alikuja nje ya nyumba ya Lucy na kuanza kumuuliza maswali kuhusu wageni waliokuja mchana .Lucy akamweleza  kwamba ni rafiki zake wa kazini .Na kila mwaka wao humtemebelea mmoja wao kwa karamu ndogo ya krisimasi .Hapo ndipo moto ulipowaka.

‘Alianza kufoka kwa hasira akisema kwamba pesa nilizotumia kuandaa mlo wote huo ni za mtoto wake-mume wangu sasa . Alipiga ukemi akiwatangazia wanakiji jinsi nilivyoolewa katika boma lake ili kuiletea familia ile hasara’ Lucy anasema .

Bullet Hole: Je,Kenei alijiua au aliuawa? Aliyefyatua risasi ni nani?

Kwa hasita Lucy pia alianza kujibizana  na mama mkwe wake akimtupia jibu la kila tusi na hapo ndipo  kilipompanda  mama mkwe akavua nguo na kusalia uchi wa mnyama ! katika mila zao ,mama mkwe ni mtu wa heshina hafai kuonyeha tupu yake kwani huchukuliwa kama laana Yote hayo yakifanyika  mume wake Lucy hakuwepo kwa sababu ya kazi yake .Kutokuwepo kwake pia kulizidisha masaibu ya Lucy  kwani katika lile boma ilionekana kama fahali wawili ambao hawangeweza kuishi katika zizi moja . Ufupisho wa kisa ni kwamba mwaka ulipoanza .Lucy alilazimika kuhaia mji wa karibu ili aishi mabli na mama mkwe aweze kupata amani .‘Mwaka huu wa 2020 nimeamua kwamba ili kuwa na amani .kimya ndio kinga yangu’ anasema Lucy kwa mkato wa kibusara . Umeyashuhudia yepi  ya sarakasi na malumbano kati ya  wanawake na mama wakwe zao? Tuambie .

Photo Credits: Radio Jambo

Read More:

Comments

comments