'Achana na sideshows hazileti shangwe.' Arrow bwoy amwambia Nadia Mukami

mukami
mukami
Mwanamuziki Arrow bwoy amezungumza kwa mara ya kwanza akimshauri msanii mwenzake Nadia Mukami. Arrow Bwoy alimwambia kuwa aachane na Sideshows ambazo hazimsaidii katika sanaa ya muziki.

Kwa muda saa, Nadia amekuwa akitoa vibao akiwashirikisha wasanii wenzake mbalimbali, lakini kwa maoni ya Arrow Bwoy azingatie sanaa ya usanii wake.

Uvumi umekuwa ukienea hapa na pale kuwa wawili hao ni wapenzi ambapo walikataa. Hii ni baada ya kutoa kibao cha 'radio love' pamoja baadae wawili hao walikiri kuwa uvumi huo ulikuwa wa ukweli ilhali mapenzi yao hayakutoboa.

“He’s an amazing friend. We tried dating but it didn’t work." Nadia Alisema.

Nadia alizidi na mazungumzo na kusema kuwa Arrow Bwoy aliendelea na maisha siku mbili tu baada ya kuachana.

Msanii Arrow amekuwa akikwepa drama hizo, lakini amezungumza akimshauri azingatie malengo yake.

"I’ll give some advice to Nadia Mukami. She is one of the vibrant female artistes in East Africa. She has so much potential in raising our Kenyan  flag high. However, she can only reach these heights once she channels all her energy into her craft." Alisema Arrow Bwoy.

Alizidi na kusema kuwa yeye ni shabiki wa Nadia na anapaswa kutilia maanani usanii wake,

“Aachane na hizo sideshows, hazileti shangwe yaani. Because the Nadia I know is the one I did a collabo with and I love the fact that she is a go-getter. Piga tu kazi. I’m your fan." Arrow Bwoy Alizungumza.