Achaneni na sisi please! Babake Brenda Cherotich aliyepona Covid 19 awarai wakenya

Msichana aliyepona virusi vya Corona na kutumiwa na serikali kama kielelezo cha kuondoa hofu kuhusu virusi hivyo Brenda Cherotich amejipata pabaya baada ya  wanamitandao kuanza kumsaga kote huku picha zake akiwa  uchi pia zikianikwa peupe .

Kando na familia yake kuwa na wakati mgumu baad ya binti yao kuambukizwa virusi hivyo ,wamejipata tena katika mashaka mengine kujaribu kuwazuia wanamitandao kumuingiza kichaa mrembo huyo ambaye wengi walianza kutilia doa masimulizi yake kuhusu jinsi alivyopata ugonjwa huo .

Babake Brenda Peter Rono  amesema familia yake kwa sasa ipo katika tahadhari ili kumuzia binti yake asiambukizwe tena virusi hivyo . Amesema familia  hiyo haitaanda karamu ya makaribisho huko Ainamoi kwa sasa ili kuzuia mkusanyiko wa watu wengi .

Bwana  Rono pia anahofia usalama wa mwanawe mwingine wa kiume ambaye yupo nchini Marekani  lakini hajapatikana na virusi hivyo.