Achapisha picha za uchi mtandaoni, Aburuzwa kortini kujibu kesi

seif
seif
Mwanamume mmoja  ameshtakiwa kwa madai ya kupiga na kusambaza picha za aliyekuwa mpenzi wake akiwa uchi kwa mitandao ya kijamii.

Mshukiwa Omar Seif alifika mbele ya hakimu mkaazi Martin Rabera siku ya Jumatatu  na kukanusha mashtaka na kuachiliwa kwa dhamana ya shilingi laki moja.

Soma hadithi nyingine:

Seif aliiambia mahakama kwamba anaugua maradhi ya Hania na alihitaji kufanyiwa upasuaji katika .

Hakimu alimuuliza kama alikuwa tayari kuapishwa kwa sababu alionekana kuhisi uchungu na akaambia mahakama kuwa hangeendelea na kesi.

Mahakama ilimuagiza kwenda kupata matibabu.

Seif aliiambia mahakama kwamba alikuwa tayari anapokea matibabu na alihitaji kupelekwa hospitalini kila asubuhi na jioni kudungwa sindano, alisema tayari alikuwa amekosa sindano moja kwa sababu ya kuwa mahakamani.

Mkurugenzi mkuu wa vuguvugu la Sisters for Justice Naila Abdallah amesema kwamba visa vya watu kudhulumiwa kupitia mitandao vimeongezeka marudufu na wakati mwingine huchangia baadhi ya wahasiriwa kujitoa uhai.

Soma hadithi nyingine:

Alisema kwamba visa vingi huwa haviripotiwi kwa sababu wahasiriwa huhofia jambo hilo kusambaa hata zaidi au kufikia familia zao na marafiki na kuamua kunyamazia.

Abadalla alisema kwamba visa vitano vimneripotiwa katika ofisi zao.

Visa hivi vingi huathiri wanawake na wasichana hasa wanafunzi wa vyuo vikuu.

Alitoa wito kwa wanawake kuwa makini sana wanapokuwa katika uhusiano.