Acheni kuchukua mikopo ili kufanya harusi kubwa-Bien awashauri Wakenya

Msanii  wa kundi la Sauti Sol Bien Aime Baraza  amewashauri  wakenya kukoma kuchukua  mikopo ili kufanya harusi kubwa na baadaye kujiweka katika madeni makubwa .

Bien alifunga ndoa ijumaa iliyopita na mpenzi wake Chiki Onwukwe katika hafla ya waalikwa pekee ambayo imedaiwa kugharimu kiasia kisichozidi shilingi laki tatu .

Wazazi wa pande zote mbili walipata fusa ya kujuana zaidi kama vile baba wa Bien na babake Chiki.

"Tulikuwa na wakati mwema kati ya familia hizi mbili,baba yangu alipata fursa ya kujuana na baba yake Chiki, kwa sasa wanajuana zaidi." Bien Alisema.

Ushauri wake kwa wanaopanga harusi na ndoa, alisema wapamge kulingana na uwezo wa mfuko wao.

"Tafadhali usifanye harusi ili kuwapendeza wazazi wako, fanya harusi kulingana na kiwango cha mfuko wako, hurusi ni mwanzo wa maisha yako

Kwa hivyo usitumie pesa zote kupanga harusi, panga harusi ndogo na ambayo unaweza ni afadhali utumie pesa zako nyingi katika fungate yako lakini si kwenye harusi." Alisema