Acheni mchezo! Wabunge wa Tanga Tanga waambia Wamalwa na Oparanya kwa kumtembelea Gideon Moi

Tanga-Tanga-MPs-730x414
Tanga-Tanga-MPs-730x414
Huku siasa za urithi zikiwa zinaendelea kushika moto na baadhi ya wanasiasa wakiendelea kunyemelea ukanda wa Magharibi mwa Kenya,wabunge wa Tanga tanga wanaoegemea upande wa naibu rais walipeleka kambeni zao maeneo hayo na kukejeli hatua ya viongoxzi kutoka upande huo kumtembelea seneta wa Baringo Gideon Moi .

Wakizungumza wakiwa katika boma la mbunge wa Bumula Mwambu Mabonga,kaunti ya Bungoma ,wabunge hao walitaja hatua hiyo kama ya kitoto na isiyostahili.

Kwa upande wake mbunge Kimilili Didmas Barasa ,alisema waziri wa Ugatuzi nchini na Eugene Wamalwa na gavana wa Kakamega Wycliffe Oparanya wanampigia debe kiongozi wa chama cha Kanu Gideon Moi eneo hilo.

Wamlwa na Oparanya waliwaongoza viongozi kadhaa kutoka magharibi kuzuru boma la Moi ambapo waliandamana na katibu mkuu wa chama cha COTU Francis Atwoli na kufanya mkutano na seneta huyo wa Baringo.

Seneta wa zamani wa Kakamega Bonny Khalwale ambaye anawania kiti cha ugavana eneo hilo amewarai viongozi Musalia Mudavadi na Moses Wetangula kujiunga na DP Ruto ili kubuni serikali mwaka 2022.

Upande wake mbunge wa Bumula Mabonga amesema eneo hilo halitamuunga mkono tena kiongozi wa ODM Raila Odinga baada ya kuwa kizingiti cha maendeleo eneo hilo.