Adhabu ya kifo ya mwanaume kupunguzwa kwa kifungo cha miaka 20

Mwanaume mmoja aliyepatikana na hatia ya kumuuwa mke wake mwaka wa 2009 aliweza kupewa adhabu ya kifo, bali akapeleka kesi yake katika mahakama ya rufaa.

Mwanaume huyo aliweza kupewa hukumu ya kukaa jela kwa miaka ishirini chini ya mahakama ya rufaa, mahakama ya rufaa iliweza kusema kuwa kesi ya Michael Nderitu ya mauaji ya mke wake, ilikuwa mauaji bila kukusudia.

Michael Nderitu alipatikana na hatia ya kumuuwa mke wake kwa kumdunga na kisu tumboni mwake, kwa ajili ya pombe (chang'aa).

Katika hukumu wa jaji Erastus Githinji, Wanjiru Karanja na Ole Kantai walisema kuwa kulikuwa na ushahidi mzuri kuwa Nderitu na mke wake waliwza kugombana na pia kupigana.

"Baada ya kutathmini upya ushahidi, tumweza kuja na hitimisho kuwa mshukiwa amepatikana na hatia ya mauaji bila kukusudia,

"Chini ya sehemu ya mahakama ya 202 ya kanuni ya adhabu inayosomwa na sehemu ya 205 ya kanuni." Walihukumu.

Nderitu aliweza kupeleka kesi yake katika mahakama ya rufaa 2017 huku akisema kuwa alipatikana na hatia na ushahidi usiostahili, alisema kuwa mahakama ilikosea katika sheria kwa kutotathmini ushahidi wote.

Hii ni kwa sababu ushahidi wa mwenye kumshtaki ulikuwa unachanganya.

Shahidi wa mashtaka Duncan Mwenda alisema mshukiwa alikuwa na kisu, na mke wake aliweza kupiga nduru huku wakazi waeneo hilo wakivutiwa sana na nduru hiyo.

Dada zake Anne Purity Njeri na Alice Waithera walitoa ushahidi na kusema kuwa Michael alimdunga Anne tumboni na kisu huku viungo vya ndani vikitoka nje.

Waliongeza na kusema kuwa mwanaume huyo aliwatishia kuwadunga pia walipokuwa wakimzuia na kumtetea dada yao, Purity na Alice walisema kuwa wapenzi hao waliuza chang'aa na pia waliweza kunywa na kupigana mara kwa mara.

Michael Nderitu aliweza kujisalimisha kwa polisi huku akisema ameweza kuuwa mtu, polisi waliamini walipoona majeraha usoni mwake huku wakimpeleka hospitali na mwishowe kukamatwa na kufungwa.

Siku moja Nderitu alirudi nyumbani ili kuchukuwa chang'aa ili aweze kuwauzia wateja wake, hapo ndipo mke wake aliweza kumzuia kuchukua na kutika kwa nyumba.

Alimchapa mke wake kofi huku akianguka chini na kupiga nduru iliyo wafanya dada zake wawili, ndugu yake na wapwa wake kuja kuangalia ni nini kilichotendeka.

Mmoja wa ndugu zake aliweza kumpiga huku mke wake akiwa amemshika.

"Ndipo mke wangu aliweza kuchukua kisu na kunidunga katika jicho langu la kushoto, ndugu yake na dada zake walipoona hivyo walianza kunichapa, huku jicho langu likitoka damu nyingi,

"Wote waliweza kuja na miti tuliokuwa tukitumia kutengeneza chang'aa na kuanza kunichapa, nilimshika mke wangu ili hasiweze kunidunga tena,

"Lakini alijirusha mbali na mimi na akajidunga mwenyewe tumboni." Alitoa ushahidi wake Nderitu.