step mom 2

Brutal Punishment? Mama wa kambo aliniwekea sumu mara tatu –Mwanawe akafa kwa kula chakula alichonipa

Malipo ni hapa hapa duniani. Ndio  kauli  ambayo  Eliza huikumbuka kila anaposimulia maisha yake ya kuteswa  na mamake wa kambo ambaye alimwekea sumu kwa chakula zaidi ya mara mbili. Matokeo yake? Siku moja kamwekea sumu kwenye andazi.

step mom 1

Baada ya mamake kuaga dunia akiwa na umri wa miaka 11 , Eliza alienda kuishi na nyanyake wa kumzaa baba. Baadaye alipokuwa na miaka 13 babake akaoa mwanamke mwingine ambaye sasa alianza kuwa mamake mlezi. Ila mama wa kambo alikuja na makovu sana kwa sababu hakumpenda Eliza. Ukatili aliomuonyesha Eliza haukumfikia mume wake na mara nyingi madhila yake yangepita bila kuripotiwa huku Eliza akiteseka kimya kimya. Siku  nyingi alifanyishwa kazi kama punda  wa kukodishwa kuanzia alfajiri hadi  jioni bila kupata pumzi wala cha kutia mdomoni. Kwa sababu  Eliza alipendwa na wengi waliomhurumia kwa kuwa yatima, mamake alikuwa hapendi hilo na wakati mwingi ilionekana kama mashindano kati yake na mamake wa kambo.

‘Niliachwa na mke wangu baada ya kukatwa sehemu zangu za siri kwa ajili ya kansa’ Jamaa asimulia jinsi upasuaji wa Penectomy

Wakati  Eliza alivyofanya mtihani wa KCPE na kupita vizuri zaidi kwa sababu alikuwa msichana wa kwanza katika wilaya, mamake kambo alianza kumwinda ili kumuua. Angeambia hilo baba mtu hangeamini lakini hatua zake zilianza kudhihirika kwa njia iliyowashangaza wengi. Siku moja akitoka shuleni, mamake alimpa  pilau. Eliza alishangaa kwa sababu wakati alipokuwa nyumbani kabla ya kwenda shule ya upili mamake wa kambo alikuwa akimbania chakula kwa hivyo ilikuwa mshutuko kwake kukaribishwa kwa tabasamu na kupewa sahani ya pilau.Baada ya kula, Eliza alianza kuumwa na tumbo, akijing’ata kwa uchungu alishangaa kwamba mamake hakuwa na haraka za kutafuta usaidizi na hapo ndipo alipogundua kwamba kulikuwa na  kitu  katika kile chakula.

‘Mwajiri wangu alinitaka nifanye mapenzi na mbwa wake.’ Mkenya aliyekwenda Bahrain kufanya kazi asimulia masaibu yaliyompata

Kwa bahati  nzuri majirani walisikia kilio chake  na akakimbizwa hospitalini. Eliza aliponea kifo kwa  tundu la sindano.  Hiyo ilikuwa mara ya kwanza mamake wa kambo kujaribu kumuua na baadaye akajiambia kwamba hatowahi tena kumuamini au kula chochote kutoka kwake. Miaka miwili baadaye, Eliza alijipata tena katika  tukio la kushtua. Wakiwa katika party ya birthday yake, yaliletwa mapochopocho yaliyopikwa na kuwekwa katika  mabakuli makubwa ya kufunikwa vizuri. Eliza alijua labda ni mmoja wa rafiki zake alikuwa amekileta chakula hicho. Jioni wageni wakishaenda kwa sababu kulikuwa na vyakula vingi, hakuna aliyekuwa amekigusa hicho katika bakuli zilizoletwa awali. Mama wa kambo pia likuwepo kwani karamu ilikuwa ikiandaliwa katika boma la nyanyake Eliza, wakati huo mamake wa kambo alikuwa amepata mtoto aliyekuwa sasa na  miaka mitano. Katika pilka pilka za kujipakulia kile chakula, mtoto huyo ambaye sasa alikuwa kakake wa kambo alimkaribia na  Eliza akambeba akijianda kuketi ili kuanza kula. Huwezi kuanza kula wakati mtoto anapokuangalia na Eliza  alimpakulia pia na kuanza kumlisha.

Coronavirus : Walivuta matiti yangu na kusema, ‘Wewe sio mwanamke ‘

Pindi tu mtoto alipokimeza kile chakula alianza kukohoa  kana kwamba alikuwa amesakamwa. Mamake alikimbia  kuja kuangalia na  cha alichouliani iwapo Eliza alikuwa amempa mtoto chakula kilichokuwa katika  zile hotpot, Eliza alipoitikia mama alianza kupiga ukemi na papo hapo watu wakajua kwamba aliyekuwa amelengwa na chakula kile chenye sumu ni Eliza na rafiki zake ambao wangekila. Maskini kakake mdogo wa Eliza hakuweza kunusurika  na alipofikishwa hospitalini, madaktari walisema ameaga dunia. Hiyo ndio adhabu iliyompata mamake wa kambo na tangia hapo Eliza naye hawajawahi kuonana hivi.

 

 

Photo Credits: Hisani

Read More:

Comments

comments