Aduda akataa madai kuwa Ko'galo imemsajili Imanishimwe

Afisa mtendaji wa Gor Mahia, Lordvick Aduda amekataa madai kuwa Gor Mahia imekamilisha uhamisho wake Imanishimwe kutoka Rayon Sports ya Rwanda.

Akizungumza na shirika mooja la habari hapa nchini, Aduda alisema kuwa," Hatujasajili mchezaji yeyote kwa sasa. Hata hivyo, tumefikia makubliano na mchezaji mwenyewe pamoja na klabu ya yake ila hatujakubaliana matamshi yoyote ya kimkataba na klabu yake wala Imanishimwe mwenyewe."

Habari zilizoibuka jana zilikuwa na madai kuwa ko'galo walikuwa wamekamilisha usajili wa Imanishwe kutoka Rayon Sports ya Rwanda.

"Iwapo tutafanya usajili wowote basi tutawaita wote mje mwone kisha tuwape nafasi ya kumuliza mcheza maswali kuhusu maazimio yake ndani ya Gor Mahia,"Aduda alisisitiza.

Imanishimwe ndiye mfungaji bora wa klabu hio ya Rwanda huku akiwa amecheka na nyavu mara 29 huku akipika magoli 53.

Gor Mahia inatajia kumpoteza Francis Kahata anayekaribia kukamilisha uhamisho wake hadi klabu ya Simba ya Tanzania. Uhamisho wake Imanishwe ni afueni kwani atalijaza pengo lake Kahata.