Screenshot_from_2019_11_25_12_18_03__1574673547_82268

“Aendelee kuvumilia, Itabidi tu avumilie…” Dinah katika mawasiliano ya simu na Gidi.

Mkewe John Bi Dinah, 38 amekataa kabisa kurudiana na mmewe katika kipindi cha Patanisho kinachoruka kituo hiki.

Ushawishi wa Gidi na Ghost kupitia laini ya simu umegonga mwamba kuwapatanisha John na mkewe.

John ,37 amesema kuwa mamake Dina amesababisha nyufa katika ndoa hiyo ya miaka 10.

Jamaa aruka kutoka feri ya MV Harambee na kujirusha bahari Hindi Likoni

“Mamake anampotosha sana. Kuna siku amekuja kutibiwa hapa Nairobi. Wakati huo alikuwa anasema msichana wake badala ya kufanya kazi ya ofisi anafanya kazi ya biashara. Kwa ufupi hanitaki…” alisema John.

“Matatizo yalianza mwaka jana mwezi wa Agosti lakini mwaka huu mwezi wa Machi tukakosana…” John amesema.

John na mkewe wamebarikiwa na watoto 3.

Aidha, jamaa huyu amesimulia A-Z jinsi masaibu yalivunja mapenzi yaliyojengeka kwenye misingi ya upendo.

Size 8 afunguka mengi kumhusu babake, alivyotoa msaada kipindi cha ujauzito

“Nilitafuta jamaa ambaye walikuwa na mpango wa kando na mke wangu. Akaeleza uhusiano wao. Nikauliza bibi pia akakubali. Kitu hiki kiliniudhi sana lakini sikumdhuru mwanaume huyo…” Alifunguka John.

Mkewe hakuonyesha dalili za kupatana na mwanamume huyu.

“Aendelee kuvumilia.Atangoja tu. Itabidi tu avumilie…” Dinah katika mawasiliano ya simu na Gidi.

Baada ya juhudi za wawili hawa kupatana kugonga mwamba, Gidi na Ghost wamewataka wasikilizaji kutoa maoni na kutuma jumbe za kumtuliza John.

Je, una maoni gani? John aoe bibi mwingine ama azidishe juhudi za kumtafuta Dina?

Photo Credits: FILE

Read More:

Comments

comments