AFCON: Mabingwa watetezi Cameroon waanza vyema, Ghana walemewa na Benin

cameroon
cameroon
Cameroon walianza kampeni yao ya kutetea taji la AFCON na ushindi wa 2-0 dhidi ya Guinnea Bissau katika mechi yao ya ufunguzi ya kundi F nchini Misri jana.

Mabao ya Yaya Banana na Stephane Bahoken katika kipindi cha pili yaliwasaidia Indomitable Lions kuwa kileleni mwa kundi hilo na alama tatu.

Wakati huo huo Ghana walitoka sare ya 2-2 na Benin katika mechi yao ya mwisho ya raundi ya kwanza kwenye kipute hicho.

Mickaël Poté aliwapa Benin uongozi dakika mbili baada ya mechi kuanza kabla ya black stars kuchukua uongozi kupitia kwa mabao ya ndugu Andre na Jordan Ayew.

Mwanariadha wa Kenya wa mbio za masafa marefu Salome Jerono amepigwa marufuku na kitengo cha  maadili ya riadha baada ya kupatikana kutumia dawa zilizoharamishwa kwenye spoti. Biwott, ambaye alipewa marufuku ya miaka miwili mwaka wa 2013 alipopatikana kutumia dawa hizo baada ya kushinda mbio za mwaka 2012 za Standard Chartered Marathon, alimaliza wa pili katika mbio za Marathon za Sao Paulo mwezi Aprili mwaka huu. Ni mkenya wa nne kupigwa marufuku kwa kutumia dawa hizo katika kipindi cha miezi miwili.

Ifuatayo ni msururu wa habari za spoti ndani ya ligi kuu ya Uingereza.

Liverpool wanapambana na vilabu vingine vikubwa vya Uropa katika kutaka kumsajili Sepp van den Berg kutoka PEC Zwolle. Bayern Munich wanaripotiwa kumtaka sana kiungo huyo wa kati mwenye umri wa miaka 17 baada ya ofa ya Sampdoria ya pauni milioni 2.5 kwa ajili ya mchezaji huyo mwezi Januari huku Ajax na PSV Eindhoven pia wakimtaka.

Hatma ya mchezaji huyo huenda ikaamuliwa katika kipindi cha masaa 72 yajayo.

Derby wameipa Chelsea ruhusa ya kuongea na Frank Lampard kuhusu wadhfa wa meneja ulio wazi ugani Stamford Bridge. Chelsea wameiambia Derby kwamba wako tayari kulipa pauni milioni 4 za ada ya kipengee cha fidia katika mkataba wa Lampard.

Lampard mwenye umri wa miaka 41 anatarajiwa kuchukua nafasi aliyoacha Maurizio Sarri baada ya Muitaliano huyo kuregea nyumbani Juventus.