AFCON: Nigeria wainyuka Tunisia na kumaliza katika nafasi ya tatu

ighalo (1)
ighalo (1)
Odion Ighalo alifunga bao la pekee Nigeria walipowanyuka Tunisia 1-0 na kumaliza watatu katika kipute cha AFCON mwaka huu.

Ighalo ndiye mfungaji bora wa kipute hicho akiwa na mabao matano. Katika mechi hiyo Tunisia walikaribia kufunga wakati Ferjani Sassi na Ghaylene Chaalali walipopiga mikiki mikubwa.

Tunisia walikua mabingwa mwaka wa 2004. Mabingwa mara tatu Nigeria sasa wamemaliza katika nafasi ya tatu mara nane sasa.

Kwingineko, Arsenal wanamsubiri meneja wa Real Madrid Zinedine Zidane kuidhinisha mkataba wa kiungo wa kati Dani Ceballos. Spurs walikua wanajadiliana na Real kuhusu mchezaji huyo lakini klabu hiyo na mchezaji huyo wanapendelea pendekezo la Gunners la mkopo, huku mkataba ukitarajiwa kuafikiwa kwa baraka zake Zidane.

Real Madrid, ambao pia awali walitaka kumuuza mchezaji huyo, sasa wanataka mkataba wa muda kutokana na mchezaji huyo kuonyesha mchezo mzuri katika michuano ya ubingwa Uropa ya wachezaji wa chini ya umri wa miaka 21.

Kieran Trippier amejiunga na Atletico Madrid kwa mkataba wa miaka mitatu kutoka Tottenham. Spurs walipewa fursa ya kumsajili mshambulizi Angel Correa wakati wa majadiliano lakini badala yake wamechagua mkataba wa pesa.

Trippier anaondoka Tottenham baada ya kuwachezea mara 114 katika kipindi cha misimu minne. Mchezaji huyo wa miaka 28 anakua wa nne kusajiliwa na Atletico msimu huu wa joto akijiunga na kina Joao Felix, Marcos Llorente na Felipe ugani Wanda Metropolitano.

Mkataba wake ulikua wa pauni milioni 21.7.

Inter Milan wana shaka kuhusu kitita cha pauni milioni 75 Manchester United inakihitaji kwa ajili ya mshambuliaji wa Ubelgiji Romelu Lukaku.

Inter imetoa ombi la mkopo wa miaka miwili, ambapo wataweza kulipa kwa awamu za Pauni milioni 9, pauni milioni 27 na pauni milioni 27, lakini United wanataka fedha zote kwa mkupuo.