AFCON: Wenyeji Misri waizaba Uganda, Congo wawakalifisha Zimbabwe

salah (1)
salah (1)
Wenyeji Misri walimaliza rekodi yao ya asilimia 100 katika kipute cha AFCON kinachoendelea na ushindi wa 2-0 dhidi ya Uganda na kufuzu kwa raundi ya 16 bora.

Kiungo wa Liverpool Mohamed Salah alianza kufunga kabla ya nahodha El Mohamady kuongeza bao la pili. Kwingineko DR Congo waliwanyuka Zimbabwe mabao 4-1 kupitia kwa mabao ya Cedrick Bakambu. Congo walimaliza watatu wakiwa na alama tatu, alama moja nyuma ya Uganda ambao pia walifuzu.

Madagascar walipata ushindi wa kushangaza zaidi katika kipute hicho kufikia sasa walipowanyuka Nigeria mabao 2-0. Lala alianza kufunga kabla ya Carolus Andriamatsi kuongeza bao la pili na kuwasaidia kumaliza na alama 7 alama moja juu ya Nigeria ambao pia wamefuzu.

Guniea waliwafunga Burundi mabao 2-0.

Ifuatayo ni msururu wa habari za spoti duniani.

Faith Kipyegon aliregea kutoka likizo ya kijufungua na kushinda mbio za mita 1500 za IAAF Prefontaine classic huko Oregon, kwa dakika 3 na sekunde 59.

Alimpiku Laura Muir wa Uingereza Shelby Houlihan wa Marekani. Mkenya mwingine Beatrice Chepkoech alishinda mbio za mita elfu 3 za kuruka viunzi kwa dakika 8 na sekunde 55, na kumaliza mbele ya Emma Coburn aliyeibuka wa pili.

Katika kabumbu, Juventus wanatarajiwa kukamilisha usajili wa kiungo wa kati wa Ufaransa Adrien Rabiot katika kipindi cha masaa 48 yajayo.

Mkataba wa mchezaji huyo wa umri wa miaka 24, Paris St-Germain ulitamatika jana na kumwacha kua huru kusajiliwa na vilabu hasimu. Kocha wa PSG Thomas Tuchel alidinda kumchukua mchezaji huyo Disemba mwaka uliopita baada ya kuibuka kwamba alitaka kuondoka.

Atakua mchezaji wa pili kusajiliwa na Juventus msimu huu wa joto, baada ya Aaron Ramsey kuwasili kutoka Arsenal.

Huko Uingereza, kocha wa Manchester City Pep Guardiola amesema hana uhakika kama Neymar mwenye umri wa miaka 27, atakuwa na makali yale yale aliyokuwa nayo kabla, atakaporejea klabu ya Barcelona akitokea klabu ya Paris St-Germain.

Kwingineko Manchester United wameshaafikiana kuhusu matakwa binafsi na mshambuliaji wa Sevilla Wissam Ben Yedder. Mshambuliaji huyo raia wa Ufaransa anatarajiwa kujiunga na mashetani Wekundu endapo mshambuliaji wa Ubelgiji Romelo Lukaku atauzwa ama la.