Afika GPO na umaskini, Hii leo CEO wa Njue Foundation

IMG_0248__1568808716_81349
IMG_0248__1568808716_81349
Njue amesimulia hadithi yake inayovutia masikio ya wengi.

Jamaa huyu amekulia katika familia ya watoto 12 na iliyojawa na umaskini tele.

Soma hadithi nyingine:

Haya ameyasema katika Bustani la Massawe.

"Nilikuja Nairobi na seepers. Nilikuwa na miaka 19 baada ya kidato cha nne."

"Baada ya kidato cha 4 nikaona nifike mjini.Tulikuwa wengi hatungesoma sana. Familia ya watoto 12. Yeye ni mtoto wa 8."

Alipofika GPO, Njue aliipiga simu ya Jamii katika shirika la reli alipokuwa akifanya kazi bwana wa dadake.

Soma hadithi nyingine:

Kilichowafanya dadake na bwana kukasirika na kufanya dalili za kumfukuza Njue ni kwamba hakua ametoa taarifa ya kuwatembelea.

"Tukaanza kuishi pamoja. Alibadilika chakula kwa sababu ni budget. Ata mimi nikaanza kuona nimeharibu budget ya hiyo familia."

'Dadangu aliniuliza maswali mengi. Anashindwa vipi niliamua kuja kwake."

Soma hadithi nyingine:

"Alikuwa na watoto 3. Nikaoana vile ananipimia. Aliambia dadangu aidha aamue nirudi nyumbani ama anitafutie pahali pa kuishi."

Baadaye Njue alipata kazi iliyomlipa shilingi 250 kwa siku na kuamua kuanzisha mpango wa kuwasaidia watoto yatima.

"Nilianza na watoto 3 ambao hawakuwa na baba na mama yao alikuwa anateseka. Nilihakikisha kuwa wameenda vyuo vya kiufundi."