Afisa shujaa Japheth Nuru afanyiwa misa yake All Saints Cathedral

Ni shambulizi lililosababisha vifo vya watu 21 na zaidi ya watu 170 kuokolewa kutoka mikononi mwa maigaidi.

Milio ya risasi ilisikika katika hoteli wa DusitD2 na damu za wananchi wasio na hatia kumwagika kwa hali hiyo, pia polisi kupoteza wenzao katika pambano hilo kati ya polisi na magaidi hao.

Kati ya polisi waliofariki afisa mmoja wa recce amefanyiwa misa yake leo eneo la all saint cathedral kaunti ya Nairobi.

Nuru alisimuliwa kama afisa mkarimu, mwenye kujali na mwenye moyo mkubwa.

Msemaji wa serikali Erick Kiraithe aliwaongoza maafisa wa serikali ilikumsifu shujaa huyo aliyepoteza maisha yake akiwalinda wananchi wa kenya.

"Japheth Nuru alikufa kama shujaa alikufa ili wananchi wengine waweze kuokolewa kifo cha papo hapo."

"Lengo la gaidi ni kuuwa watu wengi iwezekanavyona na tuna washukuru pilisi wetu kwa majibu ya haraka." Alisema Kiraithe.

Mbunge wa Taita Taveta Naomi Shabaan alimtambua Nuru kama afisa mwenye heshima aliye kuwa anajitolea kwa mambo mengi na kuhakikisha  yako bora.

Nuru atazikwa kesho nyumbani kwake kaunti ya Taita Taveta, Mkuu wa polisi Joseph Boinnet jumatano alikanusha madai ya kwamba familia ya Nuru haijatengwa.

Aliongezea kuwa polisi itasimamia mahitaji ya mazishi ya maafisa waliofariki.

"Tutawalipia gharama zote za mazishi kwa maafisa waliopoteza maisha yao wakiwa kazi kwa huduma yetu.

"Nimepeana amri kuwa mwili wa mwendazake Japheth kupelekwa nyumbani kwake na ndege ya polisi kabla ya kuzikwa kwake jumamosi." Boinnet alisema.

Pia aliongezea kuwa vijana wa (NationalYouth Service) wanajenga nyumba kwa sababu ya familia.

Nishambulizi ambalo litaishi akilini mwa waathiriwa na kuacha wengu mayatima, wajane na pia wengi kwa mshtuka usio wa kawaida, kama vile shambulizi la Westgate lililofanyika miaka mitano iliyopita.