Afrika Kusini imesajili visa 101,590 vya maambukizi kufikia sasa

Taifa la Afrika Kusini likiwa ni miongoni mwa mataifa ya Afrika,linaendelea kusajili idadi kubwa ya maambukizi huku kufikia sasa ikiripotiwa kuwa taifa hilo limesajili visa 101,590 vya maambukizi.

Vile vile taifa hilo limewapima watu 1.3 kuhusiana na vipimo hivyo ambapo ni asilimia 34.3 ya maambukizi.

Kufikia sasa bara la Afrika limesajili visa 318,321 vya maambukizi huku watu 153,242 wakiwa wamepona .

Watu wengine 8,371 wamepoteza maisha kutokana na virusi hivyo.

Visa milioni 9.19 vimeripotiwa kote ulimwenguni kufikia sasa huku watu milioni 4.96 wakiwa wamepona .

Aidha watu wengine 474,503 wanaripotiwa kuaga dunia kutokana na virusi hivyo.