Afrika Kusini kufungua shule Jumatano ijayo - Pata mkusanyiko wa habari hii na nyingine

EWwvnOaXYAIcg_C
EWwvnOaXYAIcg_C
NA NICKSON TOSI

Taifa la Afrika Kusini limetangaza kuwa litafungua shule zote nchini humo kuanzia Jumatano ijayo.

Taarifa hiyo inawadia licha ya taifa hilo kuongoza katika bara la Afrika na visa vya maambukizi zaidi ya alfu nne.

Kwingineko ni kuwa wabunge wa kenya sasa wanataka serikali kuwajumuisha kama watu wanaotoa mahitaji spesheli nchini wakati huu ambapo taifa la Kenya linakabiliana janga corona.

Kampuni ya umeme nchini KenGen imetoa ufadhili wa kima cha milioni 20 kwa serikali ili kusaidia kukabiliana na janga la Corona ambalo limekita kambi nchini.

Vile vile KenGen imepeana shilingi milioni 10 kwa serikali ili kusaidia ununuzi wa vitakasa mikono na vifaa vingine.

Kutokana na mkurupuko wa virus vya corona nchini na kuchangia asilimia kubwa ya kampuni na biashara kufungwa, huenda uchumi wa Kenya hautafana kamwe hata kwa asilimia 2, aonya waziri wa Fedha Ukur Yattani.

Muigizaji wa Boollywood Irrfan Khan, ameaga dunia akiwa na miaka 53. Khan atakumbukwa sana kwa filamu zake za Slumdog Millionaire  na Jurassic World.

Mwanasiasa wa zamani Kimani Wanyoike ameaga  dunia baada ya kuugua kwa muda. Wanyoike amefariki akiwa na miaka 85.

Ni taarifa tu ambazo zimegonga vichwa vya habari mchana huu.