Afrika yaandikisha visa 100,000 vya maabukizi ya Corona -WHO

Shirika la Afya Duniani tawi la Afrika WHO  linakadaria kuwa bara la Afrika kufikia sasa limesajili visa takriban 100,000 vya maambukizi huku watu 3000 wakiwa wamedhibitishwa kuaga dunia kutokana na virusi hivyo hatari.

Kulingana na WHO watu 40,000 kutoka mataifa 54 ya Afrika wameruhusiwa kuenda nyumbani baada ya kutibiwa na kupona .

Taifa la Afrika Kusini lingali kama taifa la Kipekee Afrika linaloongoza kwa idadi ya maambukizi likiwa na watu 19000 walioambukizwa.

Taifa la Kenya katika uknda wa Afrika Mashariki limesajili visa vipya 31 na hivyo kufikisha idadi ya watu walioambukizwa virusi hivyo kuwa 1,192.

Idadi ya watu walioafariki imesalia 50 huku wale waliopona wakiwa watu 380.