Afueni: Ndege mbili zang'oa nanga JKIA na wanajeshi kufanya kazi

Polisi wa kitengo cha huduma ya jumla (GSU) na polisi walipambana na wafanyakazi wa JKIA waliogoma jumatano asubuhi ili kuwa tawanya na kulazimika kutumia vitoa machozi ili waweze kutawanyika.

Afueni ilipatikana wakati ndege mbili ziliweza kug'oa nanga katika uwanja huo wa JKIA, ndege ya Kenya Airways na ndege ya Ethiopian zikiweza kupata nafasi na kisha kuanza safari.

Mkurugenzi mkuu wa KQ Sebastian Mikosz alisema kuwa ndege ishirini na nne ziliweza kukatizwa huku mbili ambazo zilikuwa zinatua ziliweza kuamua kuenda mjini Mombasa na nchini Tanzania.

"Asilimia ya ndege 80% zilikuwa za nchi za nje." Alieleza Sebastian.

Ndege mbili ambazo zilikuwa zimeamua kuenda kutua Mombasa na nchini Tanzania ziliweza kufika katika uwanja huo wa ndege wa JKIA Nairobi.

“KQ 349 from Khartoum had been diverted to Kilimanjaro. This flight landed in Nairobi at 0517hrs. KQ505 from Accra that had been diverted to Mombasa arrived at 0559hrs,” Kauli kutoka kwa kazi ya kitaifa ilisoma.

Ndege zingine tatu za London, Amsterdam na Mumbai zilitarajiwa kung'oa nanga kabla ya siku kuisha, Mikosz aliweza kuomba msamaha kwa wasafiri huku akisema kuwa wanapaswa kuwasiliana na watu halali wa ndege zao ili kujua wataweza kung'oa nanga wakati upi.

Pia alisema wasafiri wasiweze kuwa na wasiwasi kwa sababu kuna ulinzi wa kutosha katika uwanja huo wa Ndege.

Zaidi ya abiria mia moja waliweza kukwama katika uwanja huo wa ndege kwa kukatizwa kwa ndege hii inafuatia wafanyakazi wa JKIA kufanya mgomo.

Hii ni kwa sababu ya kukataa madai ya kuwa usimamizi wa JKIA utaweza kupelekwa katika sekta ya Kenya Airways, nap ia kushtumu sekta hiyo kwa kuharibu pesa.

Wafanyakazi wa mamlaka wa Kenya Airport walisema kuwa usukani huo utawaacha wengi wao wakiwa hawana mahali pa kuenda kwa sababu kazi yao itakuwa imeisha.

Ni mgomo ulio sababisha katibu mkuu Moses Ndiema kushikwa na polisi na kisha kutiwa ndani, huku kukisemekana kuwa mgomo huo sio halali.