Afueniya haraka! Tuju apelekwa Uingereza kwa matibabu spesheli

TUJU
TUJU
NA NICKSON TOSI

Katibu mkuu wa chama cha Jubilee Raphael Tuju amepelekwa Uingereza kwa matibabu spesheli baada ya rais Uhuru Kenyatta kutoa amri.

Tuju,rafiki wa karibu wa rais Kenyatta alihusika katika ajali mbaya ya barabarani jumatano iliyopita akielekea katika hafla ya mazishi ya mzee Moi Kabarak kaunti ya Nakuru.

Taarifa tulizodhibitisha ni kuwa Tuju alisafirishwa hadi uwanja wa ndege wa JKIA usiku wa kuamkia leo.

Tuju atapokelewa Uingereza na balozi wa kenya Manoah Esipisu ,licha ya kuwa hospitali ambayo anapelekwa haijafahamika wazi.

Ndege iliyokuwa imembeba katibu huyu wa Jubilee itatua katika uwanja wa ndege Uingereza mida ya 9;30 usiku saa za Kenya.

Alhamisi wiki lililopita ,serikali iliwaamurisha mawaziri watatu wakiwemo George Magoha wa Elimu,Amina Mohamed wa na Cesily Kariuki kuweza kufanikisha matibabu ya waziri huyo katika hospitali moja Karen.

“All I can say is that his condition has generally improved,” Alisema mmoja wa madaktari katika hospitali ya Karen.

Tuju anaripotiwa kuvunjika mbavu mbili,na majeraha katika utumbo wake[intestines]..

 Pia alilalamika kutoka na ugumu wa kupumua na kuwepo na hofu kuwa huenda baadhi ya viungo vya ndani vya mwili wake vilipata majeraha wakati alipohusika katika ajali hiyo baina ya matatu na gari lake.
Tuju alikuwa nguzo muhimu katika kutchaguliwa kwa yrais kenyatta wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2017.