'Afya ya Mike Sonko inazorota anahitaji matibabu!' Wakili asema

sonko (1)
sonko (1)
Gavana wa kaunti ya Nairobi, Mike Sonko anaugua baada ya kukamatwa kwake siku ya Ijumaa na anahitaji msaada wa matibabu wa dharura. wakili wake amesema.

Wakili, Harrison Kinyanjui pia amesema kuwa afisa wa polisi aliyerekodiwa akimpiga na kumdhulumu gavana huyo anapaswa kukamatwa haraka iwezekanavyo.

NI JAMBO LA AIBU KUWA HILI LILIMTENDEKEA GAVANA WETU TUNAYEMPENDA NA SASA ANAHITAJI MATIBABU YA DHARURA KWA JINSI ALIVYODHULUMIWA NA MAAFISA WA POLISI MJINI VOI,” KINYANJUI ALISEMA.

Wakili huyo alisema kuwa maafisa hao wa polisi hawakutaka kuskia vilio vya gavana huyo ambaye licha ya kusafiri hadi Mombasa kuhudhuria sherehe, pia alihitaji matibabu kabla ya saa sita mchana kulingana na maagizo ya daktari wake.

“KANDO NA KUMUUMIZA BILA HURUMA, GAVANA PIA ALINYIMWA FURSA YA KUPATA MATIBABU YAKE NA AFYA YAKE INAZOROTA,” KINYANJUI ANASEMA.

Sonko alikamatwa Ijumaa Voi akielekea Mombasa kufunga semina ki rasmi ambayo ilikuwa imehudhuriwa na baadhi ya wafanyikazi wa kaunti ya Nairobi.

Kulingana na Kinyanjui, ni makosa kwa polisi kumchukulia kama mtu aliyekuwa mbioni ila alikuwa pamoja na walinzi wake na pia alikuwa na simu yake. 

“HUWEZI KUWA UKIJIFICHA AU KUKIMBIA KAMA UNA WALINZI ULIOPEWA NA SERIKALI HUKU SIMU YAKO PIA IKIWA HAIJAZIMWA. 

GAVANA ALIKUWA KATIKA SHUGHULI ZAKE ZA KILA SIKU,” WAKILI ALISEMA.

Meanwhile, the governor has urged his supporters to remain calm and allow him deal with the current challenge he is undergoing.

Sonko, who now walks with a limp after he sustained injuries during the acrimonious arrest, has called on his supporters to remain calm.

According to Kinyanjui, the governor has urged his supporters to drop any plans to have thousands of people accompany him to court on Monday.

“HE IS COURAGEOUS AND CONFIDENT AND HAS WARNED AGAINST ANY DRAMA. WE ARE STEADFAST AND ON TOP OF THINGS. SO LET’S WAIT,” SAID KINYANJUI.

Hata hivyo, katika taarifa yake, Sonko alisema anaamini uwajibikaji kamili, haswa inapokuja suala la usimamizi wa rasilimali za umma.

“Nimesoma neno kwa neno taarifa kutoka kwa DPP ambayo inaelezea sababu za kukamatwa kwangu na hakuna kitu kinachonipa ujasiri zaidi kama kujua kuwa tuna ukweli wa kuondoa uwongo huu uliopigwa chapa,” alisema.

Sonko aliwataka wafuasi wake na wakaazi wa Nairobi kuwa watulivu wakati anashughulika na ‘ubadhirifu huu wa muda’.

“Nahakikishia kila mtu kuwa sitatishiwa na sitaingizwa kwenye mitego ya kisiasa.” Sonko alisema anasimama kwa haki na yuko tayari zaidi kwa mchakato wa korti.

“…nitatoa silaha zangu dhidi ya hawa wanaonitapeli. Kwa kweli, hamu yangu ya haki ambayo inayomulika EACC kuhusu unyakuzi wa ardhi itaendelea.
Kulikuwa na ripoti kutoka EACC kwamba Sonko alikamatwa wakati akijaribu kukimbia lakini Sonko alikana madai haya.

“Kwa nini nikimbie? Kuenda wapi na kufanya nini? Mimi ni Mkenya ambaye huwa safarini kila wakati akifanya kile kinachofaa watu,” alisema.

Kesi hiyo iko kortini huku ikitazamiwa kung'oa nanga siku ya Juamatatu.