Ah! Wacha Mungu aitwe Mungu, fahamu watu waliokuwa makanga na sasa ni watu tajika

NA NICKSON TOSI

Waswahili walisema maisha ni rangi rangile, hubadilika kila uchao.

Hapa tumekuandalia baadhi ya watu maarufu nchini waliokuwa wakifanya kazi ya Makanga kabla ya kuinuliwa maishani na Mola.

1 Patrick Igunza.

Igunza kabla ya kuwa mtangazaji wa stesheni moja ya humu nchini alikuwa anafanaya kazi kama Makanga wa matatu katika mitaa ya Thika, Kilimani na Matuu.

"Nakumbuka mimi na marafiki kama wanne hivi, tungeenda kuwa makanga katika maeneo ya Thika, Kilimani na Matuu, tulikuwa tunafanya kazi kwa bidii ili kupata pesa za kutosha," Alisema Igunza katika mahojiano.

2 Simon Kabu

Kabu ambaye kwa sasa ni mkurugenzi mkuu wa kampuni ya usafiri ya African Tours alianza kufanya kazi kama Taniboi na muuzaji wa maziwa katika kampuni maarufu za humu nchini kabla ya kufanikiwa maishani.

Kwa sasa, jamaa huyu anaishi maisha ya kifahari baada ya kusumbuka kwa muda maishani.

Mark Masai

Wengi wanaotazama taarifa za kiingereza katika televisheni moja ya humu nchini bila shaka wanafahamu jinsi bingwa huyu anakienzi kiingereza.

Kwake alianza kama Taniboi maeneo ya Industrial Area kazi waliyokuwa wanaifanya na nduguye kabla ya kubarikiwa na kuingia katika tasnia ya uanahabari.

Mwangi Kiunjuri

Alizaliwa katika familia ya watoto 12 na kwake waziri huyu wa zamani alianza kama muuzaji wa Mitumba kabla ya kuajiriwa kama mwalimu katika shule ya upili ya Kiarithiaini, kaunti ya Nyeri.

Wakati mmoja alikuwa anauza mboga katika lori lake alilokuwa amenunua ili kukimu maslahi ya familia yake.

Oscar Sudi

Oscar Sudi licha ya cheche zake za kila mara dhidi ya kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga, ni jamaa ambaye alipitia katika changamoto nyingi kabla ya kuwa mbunge wa Kapsaret .

Sudi alikuwa anauza makaa na wakati mwingine kufanya kazi ya umakanga katika magari yaliyokuwa yanahudumu maeneo ya Eldoret.

Babake mzazi alikuwa anafanya kazi kama mpishi katika chuo kikuu cha Moi

Mhariri: Davis Ojiambo